Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 7 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 24 2017-04-10

Name

Juma Selemani Nkamia

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. JUMA S. NKAMIA aliuliza:-
Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni alipotembelea Wilaya ya Chemba aliahidi kuongeza fedha za ujenzi wa Jengo la Halmashauri mpya ya Wilaya:- Je, katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga kiasi gani kuendeleza ujenzi huo?

Name

Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juma Seleman Nkamia, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, Halmashauri ilitengewa jumla shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba. Hadi Machi, 2017 fedha zote zimepokelewa na kazi inaendelea vizuri. Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali imepanga kutumia shilingi milioni 600 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi.