Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nachukua nafasi hii kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri ya Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Mawaziri wake pamoja na Watendaji wake wote wa Wizara hii kwa kuandika na kuwakilisha hotuba hii kwa ufasaha na kwa utaalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotuba hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuipongeza Wizara kwa hatua inazozichukua juu ya uendelezaji wa wachimbaji wadogo. Kama inavyojulikana kuwa kundi hili la wachimbaji ni kubwa sana katika nchi yetu kuliko kundi la wachimbaji wengine. Kundi hili linaigusa moja kwa moja jamii ya kipato kidogo ambao wanahitaji msukumo wa kipekee ili waweze kumudu maisha yao na kuweza kupunguza umaskini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu katika hili ni kuwa Wizara iendelee kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu pamoja na kuwapatia elimu juu ya kazi hii ili waweze kufanya kazi hii kitaalamu badala ya kuendelea kufanya kazi hii kimazoea. Ikiwa Serikali itawasaidia wachimbaji hawa, wanaweza kwa kiasi kikubwa kuchangia Mfuko wa Serikali kwa kumudu kulipa tozo zitakazowekwa kwa mujibu wa utaratibu wa sheria. Pia Serikali kwa kushirikiana na Wizara hii iweke mpango maalum wa malengo ya kuazimia kuwaondoa wachimbaji hawa katika ngazi ya wachimbaji wadogo mpaka kufikia kuwa wachimbaji wakubwa.