Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

Hon. Eng. Ramo Matala Makani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na wataalam wote kwa mwelekeo wa mabadiliko makubwa katika Sekta ya Madini nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kupitia Sheria ya Mabadiliko ya Mwaka 2017 ambayo sasa yanatarajiwa, yakitekelezwa vyema, yataboresha tija katika sekta ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, uimarishaji wa usimamizi wa sekta ya madini kwa mujibu wa Sheria ya 2017 (mabadiliko). Nashauri Serikali iweze kusogeza huduma za ushauri wa kitaalam, usimamizi na kadhalika na uwepo wa wataalam wa kutosha na wenye weledi stahiki kama ilivyosisitizwa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa 2011/2012 - 2015/2016 na 2016/2017 - 2020/2021.
Kwa Tunduru tuanze kwa kupatiwa Mthamini wa Madini haraka. Tunaomba Serikali iongeze/iboreshe bajeti kwa Wizara hii muhimu kwa uchumi wa nchi, iwe ni mbegu tayari kwa mavuno zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ielekeze nguvu zaidi katika madini ya vito (gemstones). Madini makuu yaliyozoeleka ni muhimu kama yale ya vito. Hata hivyo, bado kama Taifa tunahitaji kuelekeza nguvu katika uchimbaji na shughuli zote husika za madini ya vito ikiwemo uongezaji thamani. Katika kutekeleza haya, Serikali ielekeze nguvu katika maeneo yenye potential au yaliyogundulika kuwa na aina na viwango (types and quantities) za madini ya vito.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Serikali iandae/ iboreshe kanzidata ya maeneo yenye madini ya vito (aina na viwango) katika maeneo yote nchini. Tunduru inayo madini ya vito ya alexandrite ambayo kwa Tanzania, kwa mujibu wa Taarifa ya GST ya mwaka 2011, yanapatikana Tunduru, Mbulu na Nachingwea. Madini haya ni miongoni mwa yale adimu duniani ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye madini haya, nchi yetu ikiwa ni miongoni mwa nchi 10 bora zenye viwango vya madini hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, madini hayo ya alexandrite ni yenye thamani kubwa yakiwa ni ya sita duniani ikitanguliwa na red diamond, taaffeite, grandidierite, serendibite na diamond. Alexandrite ina thamani ya Dola za Kimarekani 12,000 kwa karati moja. Ni muhimu sasa kwa Serikali kuweka nguvu kubwa vya kutosha kwa shughuli za madini ya alexandrite. Tafsiri nyepesi ni kwamba maeneo yenye madini haya yapewe umuhimu katika uboreshaji wa shughuli za madini hususan madini ya vito.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tunduru, zaidi ya alexandrite inayo madini ya vito mengine ya dhahabu, dismuth na Sapphire kwa mujibu wa GST (2011). Taarifa kwenye mitandao zinaonesha uwepo wa madini ya vito zaidi Tunduru kama ifuatavyo: Chrysoberyl, chrysoberyl var; alexandrite, corundum, corundum var, ruby, corundum var, sapphire, diamond, garnet group, magnesio taaffeite ā€“ 2Nā€™ 2S, Magnesio Taaffeite ā€“ 6N 3S, spinel, tourmaline na zircon.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu ni kwamba Serikali kupitia GST ifanye utafiti wa kina vizuri zaidi ili kuthibitisha taarifa hizi. Ikithibitika, eneo la Tunduru liorodheshwe kuwa eneo lenye uwezo wa kuchangia Pato la Taifa, lakini pia Halmashauri iboreshe bajeti yake, hivyo nguvu zaidi iwekwe huko Tunduru.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla hali hii maana yake ni utafiti zaidi, vifaa zaidi, wataalam zaidi na kadhalika ambapo kwa ufupi ni bajeti zaidi. Serikali iboreshe bajeti ya Wizara ya Madini.