Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja ya Bajeti ya Serikali. Nianze tu kwa kusema kwamba nami nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya katika Taifa letu; Watanzania wanajua na Mataifa mengi ya dunia hii yanajua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba hata sisi Waheshimiwa Wabunge, tunafanya kazi nyingi katika Majimbo yetu kwa kuhamasisha tu, kwa kuibana Serikali, lakini wakati mwingine kwa kuhamasisha wananchi, zinajengwa Hospitali, zinajengwa shule, lakini barabara pia

zinajengwa na pale wananchi wanatusifia na kutupongeza na kusema Mbunge fulani katujengea barabara, katujengea shule, katujengea hospitali; wakati huo huo pesa hizo zimetoka Serikalini. Sijawahi kusikia Mbunge hata mmoja akikataa wasimpongeze. Nadhani tunakubaliana na hilo. Kwa hiyo, tuna kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii pia kumpongeza sana Waziri wa Fedha Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango pamoja Naibu wake, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji kwa kazi Nzuri ambayo wanaifanya katika Wizara yao. Vile vile nawapongeza kwa kutengeneza hotuba nzuri sana ya Bajeti ambayo inagusa maslahi ya Watanzania wote kwa ujumla. Hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande mwingine, kuna baadhi yetu tunasema kwamba Bajeti hii ni hewa kutokana na kwamba tumeweka malengo makubwa na hatukuitekeleza kwa asilimia 100. Namwomba Mheshimiwa Dkt. Mpango, Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Naibu wake na timu yote nzima, wakaze buti, tusonge mbele. Kwa sababu wanafalsafa wanasema hivi: “most people fail, not because they aim to high and miss, it is because they aim too low and heat.” Tusonge mbele Mheshimiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono Bajeti hii kwa asilimia mia moja. Ukienda ukurasa 23 hadi wa 25 wa kitabu cha Bajeti utaona mafanikio ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018 na mafanikio hayo yanatokana na matumizi ya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi trilioni nne na zaidi na kati ya hizo, utakuta zaidi ya asilimia 25 yametumika kulipia malimbikizo ya madeni ya watumishi wa Umma, Wakandarasi, pamoja na Wazabuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza sana kwa sababu hili tatizo lilikuwa limeendelea kwa miaka mingi na hii ni ishara nzuri na ni mwanzo mzuri sana kwamba sasa tutakuwa tunapambana na malimbikizo ya madeni. Naomba tuendelee hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe shukrani zangu kwa Serikali kulipa fedha za Mkandarasi ambaye alikuwa anatekeleza Mradi wa Mkwiti Group Water supply Scheme alikuwa akidai advance ya shilingi bilioni 400 lakini amelipwa zaidi ya bilioni 300 na hivyo itamwezesha kuendelea na mradi wa maji katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwamba suala la kutatua tatizo la maji katika Halmashauri ya Tandahimba limepewa kipaumbele na kwa kweli wananchi wa Tandahimba wanashukuru sana, kwa sababu Wilaya hii ya Tandahimba ina watu zaidi ya laki 243 na tatizo la maji ni kwamba upatikanaji wa maji ni asilimia 24 tu katika vijiji, ambacho ni kiasi kidogo sana, iko chini sana na ile average ya Kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana Wizara ya Maji ielekeze nguvu zaidi katika eneo hili kwa sababu mwaka jana walikuwa wamepangiwa bajeti bilioni 2.3 na kwa sasa wanaomba Mkandarasi huyu apewe bilioni moja kwa ajili ya certificate ili kusudi aweze kumaliza ile phase one (I).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri pia inaomba wapewe kibali cha kuendelea phase II na phase III ambayo inatarajiwa kutoa huduma kwa takribani wananchi elfu 36 ambao ni asilimia 14, kwa hiyo ukichanganya na zile 24 tutaweza kufikia asilimia 38.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana wadau wa sekta ya maji tusimamie vizuri miradi yetu ya maji kwa sababu Kamati ya LAAC tumetembelea katika maeneo mbalimbali. Katika Halmashauri mbili ambazo tumezitembelea na tulikuwa tumeambiwa kwamba miradi hii imekamika na inatumika, Halmashauri zote mbili miradi haitumiki. Kwa hiyo ni tatizo, tunaweza tukawa tunaitupia Serikali lawama lakini pia Watendaji wanaonesha kutukwamisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono na nipongeze sana Serikali kuweka kipaumbele katika sekta ya kilimo. Sekta ya Kilimo ni muhimu, lakini ndani ya sekta ya kilimo kuna suala la lishe na ukiangalia malengo la maendeleo endelevu (SDG), lengo namba mbili ni kipaumbele katika masuala ya lishe. Kwa hiyo, niombe Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ishirikiane na taasisi mbalimbali au Sekta mbalimbali sekta ya afya, uvuvi, kilimo yenyewe, fedha, elimu, viwanda ili kusudi tuweze kuipa kipaumbele sekta ya lishe au masuala ya lishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kidogo eneo la nishati, tumeona katika kurasa hizo za hotuba ya Mheshimiwa Waziri 23 – 25 kwamba kuna bilioni zaidi ya 400 zimeenda katika kuendeleza Sekta ya Nishati, lakini kuna tatizo moja ambalo naliona kwamba kiasi cha bilioni 400 haziakisi sana matatizo ya kukatikakatika kwa umeme. Tatizo hili ni kubwa na hasa tunapokwenda na sera yetu ya Tanzania ya viwanda tatizo hili linaweza likawa ni kikwazo kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe sana kwanza niwapongeze sana Waziri na Naibu wake wanafanya kazi nzuri sana katika sekta hii, wanajitahidi sana. Kila unapowaambia tatizo lolote wana-respond haraka na ni kwa dakika chache sana tatizo linakuwa limetatuliwa ila ninachoona TANESCO haina Watendaji wazuri. Baadhi ya Watendaji wa TANESCO kwa kweli wanatukwamisha. Kwa hiyo wapitie vizuri utendaji wa watumishi wa TANESCO. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono asilimia mia moja.