Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango

MHE. JUMA OTHMAN HAJI: Mheshimiwa Spika, natoa shukrani zangu kwako kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hotuba hii ambayo ni muhimu katika nchi yetu. Pia napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika na kuwasilisha kwa ufanisi mkubwa katika Bunge hili. Katika kuchangia nafasi hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina ni miongoni mwa ofisi muhimu sana katika nchi hii. Hii ni ofisi inayosimamia mashirika na taasisi zaidi ya 260 katika nchi hii. Hata hivyo inaonekana utendaji wa ofisi hii bado hajazaa matunda.

Mheshimiwa Spika, Msajili wa Hazina inaonekana mamlaka yake katika baadhi ya mashirika au taasisi hayako vizuri. Anashindwa kukosoa na kuelekeza katika mashirika hayo, hana uwezo wa kutoa maelekezo hasa kwenye mikakati ya utendaji wa mashirika hayo. Aidha, msajili hawezi hata kushauri juu ya uongozi wa taasisi hizo, utakuta taasisi fulani ina uongozi wote wanakaimu lakini msajili anashindwa kutoa maelekezo juu ya uongozi ili kuondoa tatizo la kukaimu kwa uongozi wa taasisi fulani.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Wizara hii ni kwamba Wizara ichukue mikakati ya kumuwezesha Msajili kuwa na uwezo wa kurekebisha na kuelekeza mashirika au taasisi hizo ili ziwe za ufanisi zaidi kuliko ilivyo sasa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.