Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nashukuru sana kwa kupata fursa hii ya kuchagia mjadala huu wa Wizara ya Fedha na Mipango. Lakini cha kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na kuja hapa kuchangia hoja hii.

Nipende kutumia neno moja ambalo la msingi sana hili neno ni neno kubwa sana ingawa kwamba limo katika misemo ya kizamani, msemo huu unasema ukiona majuha wanapongezana usifikiri wamefanya la maana. Mheshimiwa Mwenyekiti, asiyojua maana haambiwi maana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kwenye Bunge hili kuna milio ya mbwa sasa hawa mbwa kama tutawatoa itakuwa vizuri, sababu nasikia milio ya mbwa, nasikia milio ya mbwa kama hawa mbwa tukiwatoa itakuwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, ahsante katika kuchangia suala hili nilikuwa niendelee na suala moja hasa hasa katika masuala ya mifuko. Masuala ya mifuko mara nyingi Mheshimiwa Waziri hapa alisema kwenye ukurasa wa 19 na 20 ya kwamba kuna uhakiki wa madeni lakini kwenye mifuko hii fedha zake haziendi kwa utaratibu ambao unaotakiwa. Tukitazama kwenye Mfuko wa Reli, tukitazama REA, barabara, maji, Bodi ya Korosho na mambo mengine kwamba utaratibu unaotakiwa fedha hazijaenda. Sasa pamoja na uhakiki tunaotaka, lakini tujue kwamba tumepanga bajeti ndani ya mwaka ni miezi 12, hii miezi 12 tukisema tunachelewesha kupeleka fedha hizi ndani ya miezi 12 ina maana kwamba uhakiki miezi 13. Lakini tumepanga kutumia matumizi ndani ya miezi 12 ina maana kwamba hatutopata tija na mifuko hii ambayo tumeanzisha.

Mheshimiwa Spika, pia kuna masuala ya property tax ambayo tulipanga. Kwa hiyo, naishauri Serikali kwamba ifanye uhakiki ndani ya miezi 12 pamoja na kulipa madeni hayo. Lakini mifuko hii kwamba imo kwa mujibu wa sheria na imo ndani ya Serikali. Kwa hiyo, Serikali yenyewe kwa wenyewe inakinzana katika kuzitumia pesa hizi za mifuko.

Kwa hiyo, tulikuwa tunaomba Waziri atueleze bayana mpango wake na mkakati wake wa uhakiki huu kufanyika ndani ya miezi 12 kwa mujibu wa bajeti yetu ya miezi 12 na mifuko hii itumike na fedha zitolewe kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, lingine refund za VAT hazijaenda shilingi bilioni 500 kwa watu wa migodi hazijaenda zinageuka zinakuwa deni, kuna refund nyingine ambazo zina deposit za industrial ya sugar, industrial ya sugar shilingi bilioni 35 hazijatoka fedha hizi zimenasisha mitaji kwa wafanyabiashara hawa. Mitaji hii ikikwama ina maana kwamba uwekezaji unapungua ajira kwa wananchi wetu zinapungua. Lakini hizi Taasisi zinaenda kukopa fedha baada ya hizi fedha zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, wanapoenda kukopa fedha hizi inamaana kwamba wanalipa interest, kwa hiyo, wanasababisha kuwa na upungufu wa fedha na wanapunguza wanyakazi. Lakini pia money multiply inapungua, ukiwa umezuia mia katika multiply effect inazuia mara tatu ina maana kwamba kwa hizi shilingi bilioni 500 na hizi shilingi bilioni 35 mara tatu yake ndiyo fedha zimekosa mzunguko ndani ya mwaka.

Kwa hiyo, tunamuomba Mheshimiwa Waziri awe na utaratibu mzuri wa kuweza kufanya mambo haya na hiliā€¦ (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru, naunga mkono hoja.