Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Leo nitaongelea jambo moja mahsusi kwamba hizi National Parks zote za Tanzania ambazo kwa sasa zipo 16, iliundwa TANAPA 1959 kwa Sheria, Cap Na. 412 na kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1959 ilianzishwa Hifadhi ya Serengeti. Hifadhi ya Serengeti na hifadhi zingine zilianzishwa kwa mujibu wa Government Notes (GN) ambapo GN wakati huo ilikuwa inataja mipaka, mabonde fulani, mlima, mto, jiwe iko specific GN. Tangu wakati huo mpaka leo haikuwahi kutengenezwa ramani ya Serengeti National Park na hifadhi zingine. Kitu ambacho kimetokea na kinaendelea ni kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii inapanua mipaka ya Hifadhi kinyume na GN. Ni jambo la ajabu sana nchi hii, tunawaonea Watanzania, tunawaonea watu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwe specific, Serengeti National Park katika Wilaya ya Serengeti inapakana na Vijiji vya Merenga, Mbalibali, Machochwe, Nyamakendo, Bisarara, Mbilikili, hivyo vijiji eti TANAPA wanakuja kuweka mipaka kwenye vijiji ambayo iko kinyume na GN. Sisi walivyofanya hivyo tukatafuta GN, tukatafuta na hiyo ramani yao tukaenda Mahakamani na tumewashinda Mahakamani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jaji alihamia site na zile beacon zilizowekwa enzi zile pamoja na namba zake Jaji alienda akaona nyingine wameng’oa, bahati nzuri nyingine walisahau kung’oa tukaikuta Jaji akaiona. Hii ni kuonyesha jinsi gani ambavyo TANAPA wanavamia na kuwanyang’anya wananchi maeneo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekit, sasa hivi nimeona wamehamia Tarime, nyie watu wa Tarime nendeni Mahakamani, GN iko wazi, inaeleza. Haiwezekani leo mkapora maeneo ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kibaya zaidi vijiji hivi vimepimwa vina ramani na vimepimwa na Serikali hiyohiyo. Kibaya zaidi inakuweje TANAPA ndiyo wanaenda kuweka beacon? TANAPA ni nani? TANAPA ni Waziri wa Ardhi? TANAPA leo wamepoka madaraka ya Wizara ya Ardhi, wanaenda kupima wenyewe? Sisi Serengeti tumesema hapana na Mahakama imetutetea imesema hapana, nyie TANAPA mlifanya makosa. Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla amka, usilale kuna watu wanafanya mambo visivyo huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa, unajua naumia sana maana wananchi wananyang’anywa maeneo yao ambayo wanamiliki kihalali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji wanapata shida leo wanakosa maeneo ya kuchungia mifugo yao, inawalazimu kuingiza ng’ombe kwenye hizo hifadhi kwa sababu wamenyang’anywa maeneo yao. Kwa mfano, Pori la Mkungunero wamepanua hekari na hekari kutoka square kilometer 10,300 mpaka square kilometer 20,000, mmemeza vijiji vya Watanzania, Wamasai wa watu ambao hawajui kula kimoro au nyumbu. Ingekuwa ni kama sisi Wakurya tunaishi na wale wanyama tungekuwa tushawamaliza lakini Wamasai watu wa watu hawajui, mmewanyang’anya vijiji, Kigwangalla wewe ni mtoto wa mfugaji, Mheshimiwa samahani . (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla ni mtoto wa mfugaji. Wengi humu mnafahamu wafugaji wanapata shida kweli kweli, sasa mnataka nchi nzima iwe National Parks au WMA’s. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Wizara naomba tuwasaidie wafugaji wapate maeneo ya malisho na…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)