Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nnianze na masoko ya mazao. Kama tunavyojua wananchi zaidi ya asilimia 80 wanaishi vijijini na kule ndipo wakulima wa mazao tofauti walipo. Kwa mfano mkulima wa mahindi anajitahidi analima, palizi, vibarua, dawa na kuvuna kwa kutumia fedha zake. Lakini Serikali inaweka bei elekezi ya kuuza mahindi na kwa sasa hivi bei ya mahindi imeshuka hadi shilingi 30,000 kwa gunia, isitoshe kama tujuavyo mahindi ya kisasa huwezi kuhifadhi bila dawa na ukitaka kuhifadhi bila dawa ni kutumia ma-tank ambayo ni ghali sana kuanzia magunia 100 tani ni shilingi milioni tatu mpaka shilingi milioni 2.8; sasa kwa kukatishwa tamaa huku mkulima anaweza kununua hiyo storage?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamekuwepo na mazao kama nyanya na matunda mbalimbali, kwa nini Serikali (Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda) visiwawezeshe wakulima kupata viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao kule kule vijijini halafu wanavipeleke kwenye viwanda vya kati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo Gairo kuna wakulima wengi sana wa nyanya wangeweza kusindika na nyanya na kupeleka kwenye Kiwanda cha Tomato Sauce kilichopo Iringa cha DABAGA, pia kuna kiwanda kinachoitwa DASH kipo Iringa lakini hakina malighafi ya kutosha na hii pia baadhi ya nyanya hazikidhi viwango, kuna haja ya wataalam (Maafisa Ugani) waende wakatoe elimu kwa wakulima na kuwashauri kuhusu mbegu bora na dawa zipi za kutumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo cha ndizi ni kati ya zao kubwa sana linalokubali katika mikoa ya Kilimanjaro, Kagera, Mbeya, Morogoro na kadhalika, lakini zao hili Serikali halijalichukulia kama zao linaloweza kutuingizia fedha za kigeni. Zao hili la ndizi kwa nchi kama Uganda wamekuwa waki-export kwenda nchi za Ulaya na zinauzwa kwa bei ya juu sana peace tano tu za ndizi ni sawa na pound za Uingereza tatu sawa na shilingi 9,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri sasa Serikali kutoa elimu pia jinsi ya ku-pack ili tuweze ku-export zao hili. Tukitumia Balozi zetu kwenye Kitengo cha Biashara watafute masoko kule ndio kazi yao. Hili liende sambamba na matunda kama parachichi, maembe na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba wa pembejeo na ukosefu wa mbegu bora hili limekuwa ni tatizo sasa. Kila hotuba ya bajeti tumekuwa tukiulizia suala hili na yote haya yanasababishwa kwa nchi kushindwa kuzalisha mbegu na viwanda vya pembejeo. Ushauri tunaweza kushirikisha jeshi, wafungwa kwa kutumia wataalam tukazalisha mbegu zetu na zenye ubora, Serikali iwajali wakulima.