Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

Hon. Alfredina Apolinary Kahigi

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, namkushukuru Mheshimiwa Waziri wa Kilimo pamoja na Naibu wako kwa hotuba yenu nzuri, napongeza Kamati ya Kilimo kwa maoni yao. Naomba Serikali iyafanyie kazi maoni haya na ushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Mkoa wa Kagera tuna kilio cha mnyauko wa migomba na ni wa miaka mingi sasa. Ni tatizo gani Serikali imeshindwa kumaliza tatizo hili? Naomba itusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima wa miwa (outgrowers) katika kiwanda cha Kagera Sugar wanauza miwa yao kwa mwekezaji, wanalipwa baada ya miezi mitatu, je, kuna uwezekano wa kumshauri mwenye kiwanda ili awalipe ndani ya wiki mbili ili kunusuru mashamba yao yasiharibike? Mkulima anamkopesha mwekezaji miezi mitatu miwa yake, kumbuka hawekewi riba yoyote, Mheshimiwa Waziri wasaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nawatakia kazi njema Mungu awasaidie katika kazi zenu.