Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Alfredina Apolinary Kahigi

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri wa Maji, Naibu wake pamoja na watendaji wote wa Wizara. Mungu awabariki sana katika kazi ngumu wanayoifanya. Tunaona wanajitahidi, lakini nina machache ya kushauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba wajitahidi sana pale wanapoona Waheshimiwa Wabunge wanapiga kelele. Ni kweli shida ya maji ni kubwa sana hasa wakati wa kiangazi, ni janga kubwa. Katika Mkoa wangu wa Kagera, Wilaya ya Karagwe ina mradi uliopata ufadhili toka India. Ni Mradi wa Maji ya Rwakajunju wenye zaidi ya miaka kama 20 na zaidi. Je, Serikali ina kauli gani kuhusu mradi huu?

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu aliusemea Mheshimiwa Marehemu Sir George Kahama, Mheshimiwa Gosbert Blandes na mpaka sasa Mheshimiwa Innocent Bashungwa, na mimi nausemea. Tunaomba jibu. Wananchi wa Karagwe wana shida sana ya maji, waonewe huruma.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia na baadhi ya Kata za Bukoba Vijijini wana shida ya maji waokolewe na adha hii ya maji.