Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi, dakika tano na mimi nitakwenda brief, hazitoshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mtaalam mmoja na mwalimu wa mambo ya kidini anasema; “the greatest mistake in life is being busy but not effective na the greatest challenge in life is knowing what to do”. Kwa bahati mbaya sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi hii ya Awamu ya Tano inaonekana iko busy sana, lakini haiko effective. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niungane na Mheshimiwa Mnyika kama kweli tuko serious, kuna Wabunge hapa wanasimama kwamba kwenye Majimbo yao upatikanaji wa maji ni asilimia 16 na bado wanapiga makofi wanaunga mkono bajeti hii. Mheshimiwa Mnyika amependekeza hapa tuunde Kamati Teule kama ambavyo na Mheshimiwa Esther Matiko amesema, kama ambavyo Mabunge huko nyuma yamefanya kwa ajili ya kutatua tatizo la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu tatizo la maji ni kubwa sana kama Serikali hii ina-syncronise utendaji wake kazi, mojawapo ya kikwazo kikubwa cha watalii kuja Tanzania ni pamoja na mambo ya hygenic. Inaonesha Tanzania kuna uchafu mkubwa hakuna maji, sasa usafi utapatikanaje bila maji? Hiyo ndiyo inatuangusha duniani kwamba kuna uchafu Tanzania, kuna kipindupindu, maana yake watu wanakula kinyesi na maji yanasababisha watu wasiugue. Sasa tunaleta utani katika masuala ya maji, jukumu pekee ambalo tunalo Watanzania ni kuondokana na bla bla za Chama cha Mapinduzi ambazo zimefanyika muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi ndugu zangu kama kweli Wabunge tunavaa na suti hapa, inaingiaje akilini kwamba matatizo ya maji kijijini mpaka Mheshimiwa Rais apige simu amuambie Katibu Mkuu wa Wizara anamuunganisha na Mtendaji wa Kijiji, tunaona ni jambo la kawaida kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Katibu wa Wizara ambaye juzi nilisema hapa wajibu wake mkubwa kusimamia hizi sera na utendaji, amekazana kwenye mitandao anagombana na maaskofu, this is a serious business, haijawahi kutokea katika nchi hii Katibu wa Wizara ana majukumu makubwa ya Wizara, badala ya kushughulika na matatizo ya maji, hivi akilini inaingiaje kwamba Katibu wa Wizara unamuunganishaje na Mtendaji wa Kijiji wakati hiyo shughuli iko kwenye Local Government? Inaonesha kwamba system ime-fail, haifanyi kazi. Tunafanya majukumu mazito tunashindwa utekelezaji wa kazi. Hili suala la maji ni serious business.