Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. JOEL M. MAKANYANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Mawaziri wote wawili kwa kazi nzuri sana mnayoifanya. Nawapongeza sana pia kwa bajeti yenu nzuri iliyowasilishwa Bungeni tarehe 23 Aprili, 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakiri sana kwamba mipango yote mliyoianisha ni mipango mizuri sana na kwamba kama ikifanikiwa kutekelezeka basi nchi hii tutashuhudia maendeleo kwa kasi kubwa. Kwa maana hii naiomba Serikali ijitahidi kupeleka fedha kwenye miradi iliyotengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe shukurani zangu nyingi sana kwa kazi nzuri iliyofanyika katika kazi zifuatavyo:-

(i) Daraja kati ya Kijiji cha Chilonwa na Kijiji cha Nzali lilifukuliwa upande mmoja na sasa mwaka huu pamoja na mvua kuwa kubwa, lakini maji yalipita juu ya daraja kwa kimo cha futi moja tu badala ya mita moja karibia na futi tatu. Hongereni sana.

(ii) Kwa ujenzi wa madaraja mawili, moja dogo na moja kubwa pale kwenye Kijiji cha Membe, ahsante sana.

(iii) Ukarabati wa barabara yote kutoka Buigiri kwenda Chamwino Ikulu, kwenda Chilonwa, kwenda Membe, kwenda Dabalo, kwenda Itiso hadi Segala, Izava umeendelea kufanyika kwa ubora mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi mahsusi:-

(i) Daraja lililopo kati ya Kijiji cha Chilonwa na Kijiji cha Nzali ifukuliwe na upande wa pembeni ambapo lipo daraja lingine (madaraja haya yanafanya kazi sambamba). Hii itasaidia kuhakikisha maji hayapiti juu ya daraja kabisa.

(ii) Lipo daraja linaingia Dabalo linahitaji kutengenezwa/kujengwa ili eneo hilo liweze kupitika bila hofu wakati wa mvua.

(iii) Lipo daraja linalopokea maji kutoka daraja la hapo juu (namba 2) linalounganisha Kijiji cha Dabalo A na Dabalo B (Igamba) nalo naomba lipewe kipaumbele (daraja hili sasa lipo chini ya TARURA).

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba uyapokee maombi yangu kwa niaba ya wananchi wa Jimbo langu la Chilonwa.