Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Alfredina Apolinary Kahigi

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru Mheshimiwa Waziri Profesa Makame Mbarawa pamoja na Naibu Mawaziri wake wawili, na watendaji wote wa Wizara, kwa kazi zao nzuri tunazifuatilia na tunaziona. Napenda kuwatia moyo Mola awazidishie nguvu mna kazi kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni, katika Mkoa wangu wa Kagera tuna madaraja ambayo ni mabovu naomba na sisi mtutizame, yatengenezwe yawe imara.

Mheshimiwa Naibu Spika, uwanja wa ndege, kiwanja ni kizuri sana kina viwango vya kutosha. Tatizo ni taa ndege haziwezi teremka usiku zinaishia Mwanza. Lakini tungekuwa na taa wasafiri wanaotoka Dar es Salaam, Arusha, Mwanza usiku wasilale Mwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu meli, sina shaka swali hili mnashughulikia. Naomba mkazane na ikibidi tuwe wa kwanza kutengenezewa meli wananchi wana shida sana muda umekwenda sana nawaomba sana sana tuwaonee huruma, mazao yetu yanaoza na kipato chetu tunategemea usafiri wa meli. Nawatakia kazi njema. Hapa Kazi Tu.