Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza natoa shukrani kwako wewe binafsi kwa kunipatia nafasi hii kutoa mchango wangu wa maandishi katika Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii pamoja na watendaji wake wote kwa umahiri wao wa kuongoza Wizara hii. Katika kuchangia Wizara hii, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali yetu kwa namna inavyowekeza miradi mbalimbali katika nchi yetu. Miongoni mwa uwekezaji unaofanyika ni uwekezaji wa simu za mkononi. Hivi sasa simu za mkononi siyo kitu cha fahari (luxury), hata wananchi wa vijijini wanatumia kwa shughuli zao. Imekuwa simu ni kitendea kazi kwa watu wote lakini bado bei za simu hizo ni kubwa sana kiasi ambacho wananchi hasa wa vijijini wanashindwa kumudu gharama hizo. Ushauri wangu kwa Wizara hii ni kwamba waendelee kusimamia bei hizi na kuzifanya ziwe rafiki kwa wananchi wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bodi za Wakurugenzi katika mashirika yetu, ni sehemu muhimu sana katika kusimamia na kuendesha mashirika hayo. Ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba ni vyema Wakurugenzi wanaochaguliwa wawe na ujuzi wa taasisi husika. Siyo vizuri Mkurugenzi wa Bodi ya TTCL awe ana ujuzi wa kilimo au daktari, hii haitaleta ufanisi mzuri. Ni vyema Mkurugenzi wa Bodi ya TTCL awe na ujuzi wa taasisi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.