Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.

Mheshimiwa Waziri mara nyingi nimekuwa nikizungumza naye kuhusu kilio changu cha barabara ya Old Moshi - Kiboroloni - Kikarara - Tsuduni. Mheshimiwa Waziri anafahamu kabisa umuhimu wa barabara ile, ni barabara ambayo KINAPA ime-identify kama njia ya kupanda mlima kwa ajili ya watu mashuhuri, lakini kwa sasa hivi barabara ile haipitiki, ni mbaya, lakini mmekuwa mkitupa matumaini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016/2017 kwenye kitabu cha Waziri alitenga shilingi bilioni 2.583; kwa mwaka 2017/2018 mkatenga shilingi milioni 811 na mwaka 2018/2019 ukurasa wa 198 mmetenga shilingi bilioni moja. Naomba commitment ya Mheshimiwa Waziri, TANROADS Makao Makuu wamesema wameshauza tender na upembuzi yakinifu unaendelea, ni lini sasa barabara ile itaanza kutengenezwa badala ya kutuwekea tu fedha kwenye makabrasha lakini hamtengi fedha hizi. Naomba atueleze ni lini sasa barabara ile itaanza ili wananchi wa kule Old Moshi waweze kufaidika ili na Serikali iweze kupata mapato kutokana na ile njia ya kupanda Mlima Kilimanjaro. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sio hilo tu lakini Moshi Airport imesahaulika kabisa. Mlisema mnatenga fedha kwa ajili ya Moshi Airport, uwanja huu ni very strategic. Wageni wakija kupanda Mlima Kilimanjaro wanaweza wakatumia Moshi Airport wakaruka wakaenda Seronera ambayo ina- save time na wakaweza kwenda mpaka Zanzibar, lakini uwanja ule sasa hivi umekuwa ni wa kulima maharage na karanga. Sasa sijui Mheshimiwa Waziri ana mpango gani maana tayari airport iko inaweza ikatumika pia kwa emergency landing. Atakapokuja ku-windup atatueleza wana mikakati gani kwa ajili ya Moshi Airport. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niongee kuhusu reli ya Dar es Salaam mpaka Arusha; sijaona katika mkakati wana mpango gani na reli ile. Tumekuwa tunalalamika barabara zetu zinaharabika, malori yanabeba mizigo mizito sana inaharibu barabara, lakini ile reli ingeweza kutumika ikabeba mizigo ikapeleka Arusha, mizigo ingetoka Tanga ambako kuna bandari ikaletwa Dar es Salaam au Moshi kwa njia ya reli. Sasa hivi tunatumia malori halafu barabara zinaharibika na tunalalamika malori yana-overload lazima ya-overload kwa sababu wanahitaji fedha, lakini tungetumia treni na kukawa na treni ya wageni pia wageni wangeweza kutumia kama scenery kwa ajili ya kuangalia nchi yetu na vivutio vyetu kupitia reli.

Mheshimiwa Naibu Spika, TAMESA ilijengwa mikoa yote ili kuokoa fedha za Serikali za kutengenezea magari ya Serikali. Tayari TAMESA kuna mashine na vipuri kwa ajili ya kutengeneza magari, lakini vimepitwa na wakati, miundombinu iko pale lakini kwa nini hawatengi fedha ili waweze kununua miundombinu ya kisasa ili gari za Serikali ziweze kwenda kufanyiwa service kule TAMESA ili kuokoa fedha za Serikali? Sasa hivi TAMESA wamekuwa ni wakala wa private sector badala ya TAMESA kutengeneza magari wamekuwa wakitoa barua wanawapa Serikali, Serikali inaenda kupeleka kwa Mchina wanaenda kutengeneza gari hizo, sasa huu siyo ufisadi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri atueleze ni kwa jinsi gani wamejiandaa kuirudisha TAMESA iweze kufanya kazi ili tuweze kuokoa fedha nyingi ambazo zinapotea kwenye private sector. Maana yake hamuwalipi kwa wakati wanaongeza 10% au pengine hawa watu wa Serikali ndiyo wanaoongeza 10% unakuta matumizi ya Serikali yanakuwa makubwa sana. Hamuwalipi wakati na wao wenyewe wamekopa benki mwisho wa siku unakuta fedha zinakuwa ni nyingi sana kwa wale ambao wanatengeneza magari TAMESA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, naomba niungane na wenzangu kuzungumzia TBA. Nyumba za TBA ni mbaya na mbovu. Sasa hivi TBA wamepewa zile nyumba za Uhindini, zilizokuwa za CDA, huwezi kuamini mtu anaweza kuishi pale. Mmewahamisha wafanyakazi kutoka Dar es Salaam mnakuja kuwaweka kwenye yale magofu, hivi huu ni utu? Mtu kaacha nyumba yake Dar es Salaam, familia yake, watoto wake mnakuja kuwaweka kwenye haya magofu?

Mimi nataka kujua Serikali mtaiwezeshaje TBA ili waweze kutengeneza zile nyumba watu waweze kuingia ndani waishi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kiisha kwa muda wa Mzungumzaji)