Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika taarifa ya mwaka ya Kamati hii. Pia napenda kuwapongeza wanakamati wote wa Kamati hii kwa kuandika na kuiwasilisha kwa ufasaha katika Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia taarifa hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Kamati kupewa semina za mafunzo. Kama inavyofahamika kuwa Kamati hii ni mpya hivyo ni vema semina za mafunzo kwa wanakamati zikapewa kipaumbele. Nashauri Serikali ni vizuri Wajumbe wakawa wanapewa semina ya taasisi fulani ambayo wanataka kuichunguza kabla ya kuichunguza ili kupata weledi wa kinachofanyika katika taasisi husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbili; utendaji usioridhisha. Kwenye ripoti ya Kamati hii imeonesha kwa kiasi fulani utendaji usioridhisha kwa baadhi ya taasisi hii. Hii imesababishwa na mambo mengi ikiwemo dhamana/ majukumu ya Serikali katika kuchangia taasisi hizi. Hivyo naomba Serikali ikaiangalie taarifa kwa makini na kujirekebisha ili mashirika hayo yaweze kujiendesha shughuli zake kwa manufaa ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.