Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kutuhakikishia juzi wakati unafungua tunaanza Bunge ulituhakikishia kuwa tusiwe na wasiwasi safari hii tuko salama tukiwa Dodoma.

Sasa naiomba na excutive nao watuhakikishie usalama tunapokuwa kwenye maeneo mengine mbalimbali ya nchi kwa sababu ni uwazi dunia yote sasa inajua Wabunge wa Upinzani na watu wengine wenye mawazo mbadala hawako salama. Sasa hatuwezi kujadili mipango katika mazingira ambayo sio salama, so please don’t shoot me, natoa ushauri, mawazo maoni yangu kwa Serikali, tubishane hoja na sio bullets, mfano tunazungumzia mipango ya kubana matumizi, lakini ukiangalia Baraza la Mawaziri limeongezeka, Mawaziri wameongezeka Makatibu Wakuu wameongezeka. Viongozi wa kawaida wana ulinzi wa kupita kiasi, Naibu Spika ana walinzi wawili, wasaidizi ambao akisafiri nao nje wote wanalipiwa business class zile ni fedha ambazo zinakatwa tiketi. (Makofi)

Mheshimiwa Menyekiti, nakumbuka Mheshimiwa Spika wakati ule ukiwa Naibu Spika nilikuwa nakuona unatembea na Katibu tu na gari moja. Lakini leo hii unakuta Naibu Spika ana motorcade ya magari kibao, Bashite ana motorcade, ana walinzi kuliko hata Waziri Mkuu. Sasa unajiuliza gharama zote hizi zinazotumuka kwa Bashite ulinzi motorcade kuliko Waziri Mkuu, ni majukumu gani aliyopewa ambayo yanalazimika apewe ulinzi wa gharama kiasi hicho?

T A A R I F A ....

MHE.JOSEPH O. MBILINYI: Hiyo sio taarifa hilo ni swali na hiki siyo kipindi cha maswali, kipindi cha maswali kimeshakwisha. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumzia mipango, lakini mipango bila utaratibu haiwezi kuwa mipango. Sasa watu wanawaka sana tukizungumza kuhusiana airport ya Chato, hamna mwenye tatizo na airport ya Chato, lakini tatizo ni namna ilivyokuja na bajeti yake na utaratibu wake ndiyo tatizo lililopo. Sasa ukiangalia kama project kama hizi inanikumbusha enzi ya Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga wa Zaire alikwenda kijijini kwake Gbadolite akajenga Ikulu ya ya vyumba zaidi ya 100. Akaja na project ya airport ya kimataifa, lakini leo vyote vile kwa sababu vilikuja/vilizuka bila mipango ya nchi vinakaliwa na popo na panya. Kwa sababu ndege gani itaenda kutua Chato Mheshimiwa Rais atakapomaliza muda wake, mnakosa muda wa kwenda Butiama kwa Baba wa Taifa mtaenda Chato? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunachozungumza hapa its not personal ni principals, mipango. Tunajisifu kupanda kwa bei ya korosho zao moja tu ambalo mazingira yake wote tunajua ni kama mazingira yaliyopandisha kahawa enzi za Mrema, Mrema akawa anatafuta credit miaka yake yote kwa kupanda bei ya kahawa, kumbe tatizo lilikuwa kwamba kulitokea ugonjwa wa kahawa huko Brazil kahawa ikawa inahitajika. Kwa sababu kama korosho imepanda bei kwa mipango vipi mipango ya kupandisha bei ya kunde, choroko, mbaazi, tunasikia sasa hivi mbaazi bei imekuwa mpaka shilingi 100. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama suala ni mipango na mikakati ya kutafuta masoko ya mazao basi tutumie maarifa tuliyopandisha bei ya korosho kufika shilingi 4,000 na mbaazi nayo ifike hata shilingi 1,500 au 2,000 ili kuondoa kilio hiki cha wakulima wa mbaazi, tumbaku, choroko na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakwenda sasa hivi tuna zunguka kuzindua barabara, lakini barabara zote ni za Mzee Kikwete, flyovers za Mzee Kikwete, Daraja la Kigamboni Mzee Kikwete Awamu ya Tano barabara pekee tunayoijua ya approve ni ile kutoka Mwenge mpaka Morocco ambayo wali-divert fedha za sherehe ya uhuru ikaenda kujenga kile kipande cha barabara, lakini barabara zote tunazozindua sasa hivi ni za Mzee Kikwete mwana dipromasia aliyetukuka Mungu ampe maisha marefu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwasihi Mawaziri hasa hawa wapya achene kushindana kwa matamko, mshaurini Rais maana yake kila siku matamko mara tunataka viwanda 100 kila Mkoa halafu ilo jukumu unampa Mkuu wa Mkoa ambaye hata allowances zile anazostahili kupelekewa azipelekwi hazitoshi kabisa. OC hamna, Halmashauri hamna fedha, leo unamwambia anajukumu la kusimamia ujenzi wa viwanda 100 huu sio upangaji wa mipango, huku ni kudanganyana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe sana Mawaziri wapya hasa vijana be humble, cool down, show your talent, will recognize and appriciate you, acheni misifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hili suala la makinikia naona hamna anayelizungumza hili ni suala nyeti ambalo kama Taifa tulikuwa tunalifuatilia sana, lakini kuna dillema nyingi sana katika taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tuliambiwa tuna tarajia kupata trilioni 400 plus kutoka kwa hawa mabwana waliokuwa wanatuibia kwamba kila Mtanzania angeweza kupata Noah moja na mafuta tungejua sisi wenyewe namna ya kupata, lakini kila mtanzania angeweza kupata noa moja. Lakini baadaye baada ya muda tunaambiwa kwamba wezi wamekubali kulipa bilioni 700 tu kutoka trilioni
400 plus na baadaye tunaanza kusikia tena jamaa wamegoma kwamba hawawezi hiyo kutoa. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hamna taarifa we turned to be the wealth laughing stock, dunia nzima inatucheka International media zina tuandika vibaya, zinamwandika vibaya Rais wetu kutokana na vitu kama hivi. Huyu mtu kama msemaji wa Serikali badala ya kukaa kusemea mambo kama haya yeye amekalia tu kufungia magazeti kwa vifungu ambavyo ni wrong. Mtu anakuja anafunga gazeti kwa kutumia kifungu namba 54(1) cha sheria mpya ya habari ya mwaka 2016 wakati ile sheria straight and direct inasema adhabu ni kifungo au faini kwa mtu a person, sio gazeti lakini Msemaji Mkuu wa Serikali anatoka anafungia gazeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, anafungia magazeti kwa kifungu ambacho ni wrong anafikiri watu ni wajinga, watu wanatafuta sheria hata kwenye mitandao wanaenda wanasoma kile kifungu ndiyo maana wanaharibu sifa ya Mtukufu Rais wa Awamu ya Tano mpaka watu wanamuita dikteta kwa sababu ya watu kama huyu Msemaji wa Serikali kwa sababu udiktekta ni ku-dictate, ni kulazimisha, unalazimisha sheria ambayo aihusiani kuchukua hatua ambayo haihusiani which is very wrong.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni jukumu la hili Bunge sasa kuwaambia hawa Mawaziri mnapokaa kwenye Baraza la Mawaziri muangalie Rais usoni na mumshauri, yule ni binadamu kama nilivyosema alikuwa anakaa kiti cha pale mi nilikuwa nakaa kiti cha pale havipiti hata viti sita/saba kutoka nilipokuwa nakaa. Tulikuwa tunaandikiana nae vinoti humu tukiwa na ishu mbalimbali, ninyi mnashindwaje kumshauri kwamba this is wrong, this right. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu inafika mahali sasa Watanzania hawaamini tena kauli za Serikali inakuwa flip-flop, Rais anasema hivi, Waziri anakuja nasema vile matokeo yake mnabaki kuwa defensive wakati mlikuwa kwenye position ya ku-offensive, tulivyoanza anza apa sisi Bunge hili kama Kambi ya Upinzani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, amekuja hapa Waziri wa Elimu, majukwaani mnasema Rais anaenda vizuri sasa hivi hakuna tena migomo wala maandamano ya wanafunzi, juzi tumeona mgomo, leo Waziri wa Elimu anakuja hapa anapiga longolongo, karatasi nyingi unamaliza miti tu, kutengeneza karatasi unaleta jangwa unamaliza miti, maelezo mengi. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala ni kwamba watoto wanaangaika mikopo juzi wameandamana na ninyi mlikuwa mnasema kwamba maandamano hakuna, mnatengaje fedha za wanafunzi 30,000 wakati projection ni wanafunzi 61,000 wanafunzi 31,000 wote waende wape waende mitaaani wakatukabe hii haiwezekani, kwa hiyo, lazima tuwe realistic kwenye mipango yetu. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, tulivyofika hapa tulivyoanza hili Bunge mambo tukasema mpaka wapinzani ni ukweli tulikuwa tunasema dah, bwana sasa huyu jamaa aliyekuja tutakuwa na hoja gani mnaleka hoja wenyewe Rais hayumo humu ninyi ndo mnatakiwa mje na vitu ambavyo vita-reflect uongozi wa Awamu Tano sisi tukose hoja lakini mnaleta hoja wenyewe tukisema mnashindwa kujibu hoja, mnatusubiri tutoke nje ya geti wakati mnaingia kwenye nyumba zetu mtupige pyuu pyuu, that is wrong, that is very wrong. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ulisema tusiulize tena…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbilinyi huo nao ni Mpango pia? (KIcheko)

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: ...za kata halafu ukiuliza unawauliza wahusika unawaambia kwamba aah, mmeanza mambo gani tena ya ku-shoot, wanakuambia aah, usijali we haumo, nani yumo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nakushuru sana.