Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametujalia kukutana leo hapa, bila yeye tusingekutana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili, nikushukuru wewe kwa kunipa nafasi hii adhimu kuweza kuchangia masuala ya Muungano wetu wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijachangia kuna mfano mmoja kule kwetu visiwani huwa tunautumia sana. Mfano huo ni wa ndege kurumbizi. Kurumbizi anapotoka kwenye kichaka chake kile anachokaa husema kichaka hiki kichaka mavi, kichaka hiki kinanuka, lakini ikifika jioni kurumbizi huyo chwii anajiingiza tena mle mle.
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wasemaji wa Kambi ya Upinzani tuliwasikia waliyoyasema lakini mengine tena tunaweza tukatumia huu mfano wa kurumbizi kwa sababu naona hawana ajenda zao. Wanasema kwamba huu Muungano umeshindwa, hauwezi kufanya kitu, lakini pamoja na kwamba Muungano umeshindwa suala la Zanzibar wanalileta kwenye Muungano huu. Sasa sijui wanakusudia wasaidiwe nini hapa ikiwa hakuna maana ya kuwepo kitu hiki, mimi sijafahamu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna mfano mwingine, nitasomesha sana mwaka huu. Kuna mfano mwingine, kule kwetu ikifika siku za kuandama mwezi ikiwa hujauona basi wewe ukilala unakujia mwezi tu, mwezi tu, mwezi tu. Wao walishindwa kushirika uchaguzi ule kutokana u-dictator wa kiongozi wao, kwa hiyo kila wakikaa hapa uchaguzi, uchaguzi. Mwezi kama hujauona utaendelea kuuota tu na huo uchaguzi mtauota tu mambo yameshakwisha na tayari tumepata Rais. Nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa tena na Wazanzibar kuendelea kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vitu vingine hivi ni lazima tuvitazame. Kuna watu inawezekana ikawa mapungufu yao ndiyo wanataka kuja kuyatatulia humu. Jana nilikuwa nikiangalia televisheni kuna mkoa mmoja ulimuita aliyekuwa Mwenyekiti wa chama fulani kwamba arudi mambo yanaharibika. Aliitwa akaambiwa kwamba mambo yanaharibika, kwa hiyo kweli mambo yanaharibika arudi akatengeneze, hakuna viongozi kule. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze tu wachangiaji wenzangu ambao wamechangia, wamechangia vizuri. Namshukuru sana kaka yangu, mimi leo nimpe jina la Daktari, Dkt. Shamsi Vuai Nahodha, kwa kuwang‟oa watu jino huku anacheka, unajua ni kazi. Kumng‟oa mtu jino huku anacheka ujue kwamba una falsafa kubwa sana halafu mtu hajijui kama anang‟olewa jino. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba huko Zanzibar kama miafaka ilipita na vyeo watu wakapeana lakini watu shida yao sio vyeo wana lao. Wamepewa watu nafasi, Makamu wa Rais, uchaguzi umepita watu wakafikiri labda watatulizana hawa lakini tumeona wamefanya nini?
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kilichobakia na anachoshauri Mheshimiwa Shamsi kwamba uchumi mkubwa usaidie uchumi mdogo ndio jambo la kulifanya hapa, hayo mengine hamna sera. Kwa hiyo, hayo mimi ndiyo nayozungumza…
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumzia masuala ya muungano, tunaushukuru sana muungano wetu. Muungano umetusaidia sana katika ulinzi na usalama wa nchi yetu. Labda kwa kuzungumzia historia ndogo katika Muungano, baada ya Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika majaribio mengi sana ya kutaka kupindua nchi. Majaribio yale baada ya kuungana hayakuweza kufanikiwa tena kwa sababu ya Muungano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nitasema sababu za kutaka kufanya majaribio ya mapinduzi hayo, kuna watu hawajaridhika na yale Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 na watu hao bado wapo.
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Uwepo wa watu hao ndiyo tatizo wala hakuna tatizo lingine. Kwa hiyo, tunashukuru kwa ulinzi na usalama katika Muungano wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Muungano wetu ni wa watu na jamii, tumechangamana na tunafanya kazi sehemu zote za Muungano. Wafanyabiashara wanakwenda huku na kule kufanya mambo yao ya kibiashara ndani ya Jamhuri ya Muungano. Hakuna mipaka ambayo amewekewa huyu labda ni Mzanzibari huyu ni Mtanganyika kutembea katika Tanzania yetu. Watu wanafaidika na uwekezaji, wanafaidika na kupata mambo ya financing, kuna mabenki yamo ndani ya Muungano yanakopesha kwa mtu yeyote yule ambaye yuko na wengine wamekopa wanajua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la kuipongeza Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni katika ile misaada ya GBS. Siyo hiyo peke yake hata kwenye busket fund na direct project ambayo gawiwo lake linakwenda vizuri, tunaishukuru Serikali. Tunashauri kitu kimoja, katika GBS (General Budget Support) sasa inaanza kupungua na tunawashukuru wafadhili. Kwa hiyo, tujaribu kuangalia mitazamo mengine ya kuweza kusaidiana katika suala hili la GBS.
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naunga mkono hoja.