Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

Hon. Mohamed Juma Khatib

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chonga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

MHE. MOHAMMED JUMA KHATIB: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata nafasi. Niseme mapema tu kwamba leo nina saumu, kwa hiyo ule wasiwasi na mashaka kwamba kila atakayesimama hapa ataangusha nondo, mimi nina saumu, kwa hiyo nitazungumza kwa upole kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niseme kwamba nampongeza sana Mheshimiwa gwiji wa siasa, waliokuwa hawamfahamu Maalim Seif niwaambie kwamba yule ni gwiji wa siasa, pale chuo kikuu tena rekodi yake mpaka leo haijavunjwa, alifanya Degree ya Political Science pamoja na International Relations. Sasa wakati tunakuja Bungeni; nataka niwaondoe wasiwasi; alituita sisi akatufunda vizuri akatuambia kwamba mnakwenda huko lakini tunataka muwe Wabunge wastaarabu. Serikali inapofanya vizuri ipongezeni na inapofanya vibaya isemeni, ikosoeni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hilo halitoshi tulipokuwa katika kikao cha UKAWA, Mheshimiwa Mbowe akarudia maneno hayo hayo. Kwa hiyo niwaambie kwamba sisi Wapinzani tutasifu pale ambapo litafanyika jambo zuri, pale ambapo mtavurunda, msitegemee sisi tutawasifu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mawaziri wameapa, tena kiapo cha Kikatiba kabisa cha kumshauri Mheshimiwa Rais, naomba hiyo kazi waifanye kwa ufanisi mkubwa. Wao kama Cabinet wana collective responsibility, wanatakiwa wayaendee mambo ya kitaifa kwa pamoja, wanatakiwa wamshauri Mheshimiwa Rais kwa pamoja na kwa hekima. Isitokee wanakaa na Mheshimiwa Rais muda wote mpaka anaondoka madarakani halafu mmoja anakuja kusema kwamba mtu anatumia muda mwingi zaidi kwenda safari za nje kuliko kwenda kumsalimia mama yake. Hivi huu muda wote waliokuwa pamoja kama aliona kwamba hilo la kwenda safari za nje ni baya zaidi kuliko kwenda kumsalimia mama yake kwa nini hakusema mapema? Hilo ni la pili (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu, niwape pole wananchi wa Tanzania hasa Tanzania Bara ambao Serikali, niseme kwa nia safi kabisa, walitegemea kuwaondolea matatizo mengi likiwemo la kukosa umeme katika maeneo yao. Kwa sababu nchi hii kabla ya Mradi wa REA ilikuwa imekatika mapande; pande la mijini pamoja na vijijini, huduma ya umeme ilikuwa iko mjini tu lakini vijijini kote kulikuwa giza tupu.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili la kuanzisha Mradi huu wa REA ni suala zuri sana, lakini nalo limekumbwa na matatizo na moja kati ya matatizo hayo ni pale wakubwa wetu wanapotuambia kwamba wataulinda Muungano huu kwa gharama zote. Wananchi wa vijijini walikuwa wanategemea mradi wa REA, na mradi wa REA ulikuwa unategemea msaada mkubwa wa MCC.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa huu msaada wa MCC umekosekana kwa sababu demokrasia hakuna, demokrasia haiheshimiwi, anayeingia kwenye uchaguzi akashinda siye anayepewa. Kwa hiyo, hili limewakwaza sana Watanzania Bara kwa ajili ya kupata umeme huu wa MCC, hilo ni la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)