Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Tundu Antiphas Mughwai Lissu

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Singida Mashariki

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, naomba nianze kwa kuzungumzia moja ya vitu ambavyo ni omission sijui ni nini kwa kiswahili, lakini kuna vitu ambavyo vinashangaza kwa jinsi ambavyo tumejisahau.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Katiba ya Kenya ya sasa hivi, vile vifungu vya mwanzo kabisa vimezungumzia nembo za taifa la Kenya; wimbo wa Taifa na maneno yake; court of arms na nembo nyingine za Taifa la Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Tanzania huu utakuwa ni mwaka wa 66 tangu tupate uhuru. Mheshimiwa Waziri utakapokuja kuzungumza hapa hebu waeleze Wabunge hawa kama kwa sheria za Tanzania (sizungumzii Katiba), kama Wimbo wetu wa Taifa unatambuliwa kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu miaka kumi baada ya kupata uhuru mwaka 1971 Bunge hili lilitunga sheria inayoitwa Sheria ya Nembo za Taifa na sheria ile inazungumzia Bendera ya Taifa na ile Bibi na Bwana (court of arms). Wimbo wa Taifa (Mungu Ibariki Afrika) siyo nembo ya Taifa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Mheshimiwa Waziri, atakapokuja kuzungumza hebu aje atuelezee usahaulifu huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, miaka 48 iliyopita kuanzia mwaka 1969 mpaka 1971 kilikuwa kipindi ambacho nchi yetu iliua uhuru wa vyombo vya habari kwa kutaifisha vyombo vya habari vya binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili gazeti la Daily News lilitokana na kutaifishwa kwa The Standard. Magazeti mengi yalikuwa nationalized. Tukaingia kwenye utawala wa kiimla kwa maneno ya Mheshimiwa Waziri hapa, kwenye vitabu vyao, nimekuja na copy hapa. Tukaingia kwenye dola la kiimla ambalo halikuwa linatambua uhuru wa habari na tumeenda na uimla huo mpaka 1984 tulipopata Bill of Rights kwenye Katiba yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bill of Rights hii ni muhimu sana kwenye masuala ya uhuru wa vyombo vya habari. Tofauti na haki nyingine, haki ya kupata habari imeondolewa kile kitu kinaitwa clawback clauses, haina clawback clauses. Uhuru wa kupata na kusambaza habari, hautegemei sheria kwa mujibu wa Katiba hii. Ukienda kwenye nyingine inasema kwa mujibu wa sheria, kwa kufuatana na sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Article 18 ya Katiba imeondoa clawback clauses, lakini unashangaa Mheshimiwa Rais anawaambia watu hadharani kwamba msifikiri mna uhuru wa habari wa aina hiyo. Not to that extent.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba yetu imeondoa mipaka ya uhuru wa habari. Kwenye haki ya habari there are no clawback clauses. Mheshimiwa Waziri atakapokuja hebu tunaomba atusaidie, haya maneno anakuwa ameshauriwa au anakuwa anajisemea tu. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii katika awamu hii, kama kuna kipindi ambacho uhuru wa habari unakabiliwa na tishio kuliko kipindi kingine chochote ni tangu mwaka 2015. Silaha za choice, kuna Sheria inaitwa Electronic and Postal Communications Act, imetumika kukamata watu wengi sana kwa sababu ya ku-execise uhuru wao wa habari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Makosa ya Mtandao na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari; hizo sheria tatu ndiyo zinazotengeneza utatu haramu kwenye masuala ya uhuru wa vyombo vya habari. They constitute the biggest threat on press freedom in this country. Ndiyo maana polisi wanatembea all over kwenye cyber space.

Ukiisema Serikali vibaya, ndani! Ukimkosoa Rais au Waziri, ndani! Nani aliyewaambia katika nchi hii kwamba the President is above the law? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nani aliyesema kwa mujibu wa sheria gani kwamba Rais hawezi akasemwa vibaya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mheshimiwa mmoja aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa nchi hii, alisema hiyo dhana kwamba Rais yupo juu ya sheria yenyewe ina-undermine Katiba. Mheshimiwa Jaji Mkuu Samata!

Sasa Bunge hili lina wajibu, msifikirie hii ni kelele ya wapinzani, Bunge hili lina wajibu wa kulinda uhuru wa habari. Mkinyamaza kimya ninyi mlio wengi, leo ni sisi, kesho ni Mheshimiwa Nape na keshokutwa ni wewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilizungumza wakati tunapitisha Sheria ya Vyombo vya Habari, nilinukuu maneno ya baba wa Rais wa sasa wa Ghana wakati Nkurumah anapitisha sheria ya kuweka watu kizuizini, anamtumia Waziri wa Mambo ya Ndani anaitwa Tawia Adamafio. Wakamwambia Tawia Adamafio, angalia unatengeneza mtego wa panya, utakukamata wewe. Kweli Tawia Adamafio alikuwa mtu wa kwanza katika historia ya Ghana kuwekwa kizuizini kwa sheria aliyoipitisha mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhalini Waheshimiwa Wabunge, hizi sheria; haya mambo mabaya ambayo yanafanyika nchi hii halafu mnayalinda yasisemwe, mnatuziba sisi mdomo mnafikiria mtashughulikia sisi; mnashughulikia Bunge hili na mkishalishughulikia hili Bunge, mtashughulikiwa ninyi wenyewe na hakutakuwa na mtu wa kuwapigieni kelele; hakutakuwa na mtu wa kuwasemea kwa sababu wengine wote tutakuwa tumenyamazishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni kuhusu wasanii wetu! Kuna kitu kinaitwa artistic freedom. Wasanii wanapotunga nyimbo, wana-exercise their freedom of speech as well. Ukiwakamata, ukawateka nyara na kuwatesa, una-violate their artistic freedom, una-violate their freedom of speech. Sasa hatujawahi kuona katika vipindi vingine vyote katika uhuru wa nchi hii wasanii wakitekwa nyara kwa sababu ya nyimbo zao, tumeiona kwa … (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.