Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga hoja mkono na kuwapongeza sana Mawaziri wote kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya pamoja na kazi nzuri ya usimamiaji wa mazingira inayofanyika. Napenda Wizara itoe pia kipaumbele cha vijiji ambavyo vinazunguka vyanzo vya maji kuhakikisha vyanzo hivyo vinatunzwa na kulindwa vizuri na wananchi hao. Wananchi hao inabidi na wao wafaidike na vyanzo hivyo vya maji kwa mfano; maji ambayo yanatumika Mkoani Tanga yanatoka Mto Zigi Wilayani Muheza. Tarafa ya Amani wanavijiji wanaokaa maeneo hayo kama Amani, Zirai Misarai, Mbomole, Mashewa, kwendimu na kadhalika maji wanayotumia yanatiririka bila kuwekwa vizuri. Hawasaidiwi kuweka maji hayo kuwa safi na salama. Ni vizuri Wizara ikashirikiana na Wizara ya Maji ili wananchi hawa wasigeuke kuharibu mazingira ya vyanzo hivyo. Wapewe motisha na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na pigeni kazi na nashukuru Mheshimiwa Waziri kufika Mto Zigi.