Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia kwa maandishi Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshukuru Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri yenye mwelekeo na dira ya utekelezaji wa maendeleo ya Serikali yetu. Katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-
Maeneo ya huduma za Kiuchumi; napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kasi kubwa ya maendeleo inayochukua kasi za maendeleo katika maeneo kadhaa kama vile umeme, barabara, reli na usafiri wa anga ni mkubwa na ni wa kutia moyo kwa Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu katika eneo hili la huduma za kiuchumi ni kwamba, naiomba Serikali kuwa makini kwa kuangalia viwango vya miundombinu hii ili kuepuka hasara za matengenezo ya muda mfupi mara baada ya makabidhiano ya miundombinu hii. Serikali
imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa matengenezo ya miundombinu ambayo mara nyingine sio ya lazima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Ahsante.