Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

Hon. Yussuf Kaiza Makame

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chake Chake

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu, pili nakushukuru wewe kwa kunipa fursa na mimi ya kuchangia hotuba hii ya Waziri Mkuu. Kabla ya kusema chochote naomba kwanza niunge mkono Hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusiana na Ofisi hii ya Waziri Mkuu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda kwenye maeneo matatu mpaka manne. Suala la kwanza nitazungumzia masuala ya general ya Bunge, nitazungumzia unit ya Bunge Sports, nitazungumzia masuala ya misaada ya Wahisani kwa Serikali ya Tanzania, nitazungumzia Ofisi ya Msajili kwa sababu hii haiwezekani kutokuizungumza kwa yeyote anayesimama upande huu kwa sasa inavyotekeleza majukumu yake, lakini na nne kama nitapata muda nitazungumza suala la uanzishwaji wa Baraza la Vijana la Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwenye issue ya Bunge. Mimi ni Mbunge wa awamu ya kwanza hii 2015/2020, wakati tunakuja hapa kwenye briefing ya kuapishwa mwezi wa Novemba, 2015 nilidhani kwamba Bunge linaloyasema linayasimamia. Tuliambiwa kwamba issue ya vitabu itakuwa mwisho kwenye meza zetu Mkutano ujao kwenye Bunge hili tuliloanza. Mwezi Novemba, tuliambiwa maneno hayo na Spika wa Bunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matarajio yangu ni kwamba, sasa hivi sisi tungekuwa tunatumia zile computer mpakato. Hizi siyo kwa mantiki ya kujionesha sisi tunatumia ni kwa usiri wa siri za Serikali, nyaraka hizi ni muhimu na kila kitu, lakini mpaka leo tunaenda mwaka wa pili, lile neno
baada ya kulisikia kwenye Briefing ya Bunge halijawahi kuzungumzwa tena.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu atakapokuja kuhitimisha haya makabrasha yanajaa humu, hebu tujitahidi basi, kwenye hili atakapokuja kuhitimisha atuambie Bunge letu linaenda electronically technological whatever! Atambie tunaenda kwenye computer mpakato au tunaendelea na hili mpaka tumalize Bunge hili la 11? Hilo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka kuzungumza kwenye maslahi ya Wabunge. Wabunge kituo chao cha kazi ni Dodoma na ndiyo mmeamua kwamba, kituo cha kazi kiwe Dodoma. Wabunge wanapotoka Majimboni wanakuja Dodoma asilimia kubwa ya Wabunge ni watu wanaoishi katika hoteli ama Guest hapa Dodoma. Tunapotoka kuja hapa tunapanga kwenye vyumba vyetu vya hoteli, sasa tukitoka kwenda kukagua miradi ya maendeleo ya Serikali tunakuwa tayari tumepanga kwenye vyumba vya hoteli, lakini bajeti tunayotengewa ni ile ya kukaa
Dodoma. Kwa hiyo, kimsingi kwenye hili tuache itikadi zetu za vyama na mambo mengine, Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunahitaji stahiki za mtu anayetoka kituo chake cha kazi kwenda sehemu nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa utaratibu tu kwa sababu tukienda Geita, huku tuna chumba, kule tuna chumba, cost zinaongezeka, otherwise mliangalie kwa namna nyingine suala hili kwa ajili ya Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Bunge Sports Club, limeongelewa sana. Tutaliongelea kwa umuhimu wake, hasa mwaka huu ambao tutapokea ugeni. Ninayeongea ni mchezaji wa Bunge Sports Club wa kutegemewa tena. Sasa tuliyoyapata hatutarajii tuyaone tena. Tunakushukuru Waziri Mkuu kwamba mambo yetu yamekua vizuri Kurwa ametoka kama Doto alivyotoka, lakini ilikuwa ni kusuguana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi ni stahiki zetu kama Wabunge hatuombi. Tunapotoka nje ya nchi ni stahiki zetu tunazopaswa kulipwa siyo kwamba ni maombi au ni huruma ya Bunge kutufanyia hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoomba sasa tunapanga bajeti hapa, mara nyingi tukiongea na Spika anasema bajeti mliipitisha ninyi na nini. Tuliangalie kwa kina suala la Bunge Sports Club hasa tukitilia umuhimu kwamba mwaka huu tutakuwa na ugeni wa East Africa kwenye
mashindano hayo ya East Africa, pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye Mwenyekiti wa East Africa. Kwa hiyo, itakuwa aibu kuja kuyapata yale tuliyoyakuta Mombasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengine, walisema akina Mheshimiwa Cosato Chumi hapa kwamba tulikuwa tunaingia kwenye magari ya Askari! Wabunge! Wanatushangaa Wakenya, eeh! Wewe Mbunge kweli? Kwa hiyo, tunatarajia mambo haya myarekebishe yakae vizuri, kwa sababu tukipata aibu Wabunge wa michezo linapata aibu Bunge na linapata aibu Taifa kimsingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nilisema nitazungumzia ni suala la misaada. Wakati Serikali hii inaingia madarakani mlikuwa mnazungumza kwa kina kwamba tutaenda kwenye kujitegemea na suala la misaada halitakuwa muhimu sana kwa Serikali hii. Tumemaliza mwaka huu wa bajeti asilimia 30 ya bajeti ya maendeleo ndio iliyopatikana na sababu zilizoandikwa kwenye mpango ni mbili tu; kubwa kwamba kuchelewa kwa mazungumzo ya wahisani ambayo kwa kumwambia Mbunge mwenye akili kama mimi hiyo haiingii akilini ndio iliyoandikwa kwenye mpango wa bajeti 2017/2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwamba miradi ya maendeleo iliyoandikwa haikukidhi vigezo. Kwa hiyo, ilikuwa haina maana kwangu, sio hoja za kimantiki zinazoingia kwa Mbunge; tuangalie kwa kina kwa nini Serikali yetu ilikosa misaada na fedha za bure kama za MCC, za bure kabisa.
Tuangalie kwa kina tusitoe hoja dhaifu kama hizi kwenye vitabu vyetu vya maandishi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Msajili; suala la Msajili limezungumzwa vizuri kwenye hiki kitabu cha Bunge cha Kamati ya Katiba na Sheria. Hii ni taarifa ya Bunge imeiagiza Ofisi ya Msajili ukurasa wa 30 imeiagiza Ofisi ya Msajili kwamba ifuate sheria, taratibu na kanuni. Kwa maana ya kwamba Bunge limeona kwamba Ofisi ya Msajili inakiuka sheria na taratibu hasa kwenye mgogoro wa Chama cha Wananchi CUF na suala la kutolewa kwa ruzuku isiyofuata utaratibu wa kiserikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa suala hili limeleta mjadala; msidhani kwamba hapa tukijadili tunafurahishana, Watanzania wanaona what is going on kwenye CUF. Huu mgogoro wanaujua what is going on, nini kilichopandikizwa na nini kinachofanywa. Lipumba humu ana genge lake la watu wawili tu and we are forty MPs from CUF. Hatuungi mkono kwa Lipumba, why tunafanya hivi vitu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hili suala ni la kuangaliwa kwa kina na Ofisi ya Msajili siyo Ofisi ya kutoa haki kama mtu amefukuzwa anaenda mahakamani na huko ndio kwenye kutoa haki wala hawezi ku…
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Yussuf.