Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Kwanza naomba niwapongeze Wabunge wenzetu wa upande wa pili ambao walioneka kwamba wamesimama na kutetea hizi hoja zilizopita siku mbili kama Mheshimiwa Hussein Bashe na wengine, nawaomba waendelee hivyo na kesho kwenye Muswada wa Sheria ya Habari kwa sababu nao ni disaster kwa Taifa. Kwa hiyo, nawashukuru sana na tuendelee kuwa pamoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wamarekani wanasema uchumi ni mahesabu (arithmetic’s) hautaki maneno maneno, mara uchumi umekua kwa 7.9%, mara 7.2%, uchumi ni arithmetic’s (mahesabu). Humu ndani katika retreat ya kwanza kabisa nilisema, I was scared of the future, now this is the future I was scared about ambayo wote tunaijadili. Nilikuwa mtu wa kwanza kuongelea in detail matatizo ya bandari yaliyotokana na Single Custom Territory. Nikafanya consultation mpaka na Waziri Mkuu maana alikuwepo, lakini mpaka sasa hivi hakuna kilichotoa majibu zaidi ya kusema hata meli moja ikija bandarini haina tatizo. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niendelee kusisitiza kwamba we should take jets kwa sababu lazima tuwe na international interactions. Nashukuru Mkulu ameanza kutoka, juzi alikuwa Nairobi, nafikiri ataongeza mileage kwenye ndege. Kwa sababu hata Wabunge wanaposhindwa kusafiri kwenda kwenye vyombo ambavyo ni vya makubaliano ya Kimataifa, hatuwezi kwenda SADC, PAP, tunasikia hata Spika ananyimwa kibali cha kusafiri, sasa hii nchi tukijifungia ndani humu tutapata vipi maarifa, tutabadilishana vipi mawazo na wenzetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Marekani ambao wana kila kitu bado Obama anasafiri anakuja mpaka Kenya na Tanzania kwa sababu international interactions zinakuwa ni kwa maslahi mapana. Watu hawawezi kuwa wanakuja kwetu tu, Wabunge wanakuja kwetu, delegation zinakuja kwetu na sasa hivi naona Rais anapokea delegation nyingi nyingi lakini sisi hatutoki, wataacha kuja watasema hawa tunawatembelea wao hawatutembelei, acha wajifungie humo humo ndani watajijua wenyewe, sasa hii itakuwa mbaya zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisisitize, hatuwezi kuwa na mipango bila sera. Nataka Waziri wa Fedha aniambie leo ni nini sera yetu kuhusu misaada kutoka nje? Maana tunasikia kauli nyingi za majigambo, tuna wa-criticize Wamarekani, Wazungu kwamba wenyewe hawajafanya hiki na kile, hatuhitaji misaada tuko tayari kujitegemea, lakini eventually tunaishia kuomba msaada Morocco ambao ni third world wenzetu! Morocco ni dunia ya tatu wenzetu tunaomba msaada sijui watujengee uwanja na vitu gani sijui. Labda pengine tukiangalia ngozi nyeupe tunajua kila mtu mweupe ni Mzungu na ana hela, lakini Morocco ni third world ndugu zangu na wao wanahitaji misaada kama sisi, wale ilitakiwa tuongee mambo yao mengine tu kwa sababu yule bwana ni rafiki mzuri sana wa Puff Daddy wa Marekani na hata picha zimeonesha lifestyle yake. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasema uchumi unakua uchumi unakua kwa nani? Biashara zinakufa, Mpango inabidi ubadilishe jina kwa sababu you have to live your name, kama wewe ni Mpango basi uwe na mipango. Mimi Sugu hata ukiangalia nikikomaa na kitu nakomaa nacho kama sugu, Iam living my name. Kwa hiyo, unatakiwa Mheshimiwa Mpango uishi kwa jina lako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimuulize, fedha hamna, hivi ni yeye Mpango alimshauri Rais kwamba wachapishe noti mpya kwamba watu wanaficha fedha? Watu wakificha fedha hawawezi kuficha fedha hizi ambazo zinashuka thamani kila siku, wakificha fedha wataficha dola na kadhalika. Tatizo linalotokea ni kwamba wamekusanya fedha zote za Serikali kutoka kwenye mabenki wamepeleka BoT wakati wao hawazungushi fedha wanakaa tu. Rudisheni zile fedha CRDB, NMB, NBC wale ndiyo wanaofanya biashara waendelee kukopesha, watu waendelee kufanya biashara na kutanua mambo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye ukurasa wa 14 wanasema misingi ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa 2017/2018, halafu namba nne wanasema, katika mikakati inayotarajiwa kuweka bajeti ni kusubiri bei za mafuta katika soko la dunia zinavyoendelea kuimarika. Sisi hatuchimbi mafuta, bei ya mafuta inaposhuka ni faida kwetu. Juzi nilikuwa naangalia Waziri wa Fedha wa India anasema uchumi wa India una-boom, construction zinaendelea, viwanda vinajengwa, tunachukua advantage ya kushuka kwa soko la mafuta kwa sababu sisi hatuchimbi mafuta.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watasema mafuta tunayo yatapatikana leo? Hiyo gesi imeshaanza kuchimbwa lakini bado hatuoni hata manufaa yake, mpaka leo ukienda Mtwara watu wanachoma vitumbua, watu wamechoka wanategemea korosho wakati gesi ipo na ndiyo maana hata Mheshimiwa Mwambe amechoka kugombea gesi, humsikii anasema gesi, yeye anazungumzia korosho tu. Hata watu wa Mtwara ukiwaambia gesi wanakwambia ninayo tumboni, wanaleta utani, they joke about it kwa sababu they don’t believe about it. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sisi leo hatuwezi kusema kwamba eti bajeti yetu itatengemaa kutegemea kuimarika kwa bei ya mafuta duniani. Kuimarika kwa bei ya mafuta duniani ni disaster kwetu. Faida kwetu sisi tena msimu huu ambao tunasema tunataka kujenga viwanda ni kukomaa kipindi hiki kuanzisha hivyo viwanda kwa sababu nishati ya mafuta bei iko chini na hamna namna nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasema mipango, tutapeleka milioni 50 kila kijiji, za nini? Hii ni mentality ya rushwa wakati wa uchaguzi! Ndiyo maana story zinaendelea, milioni 50 kila kijiji, milioni 10 Wabunge, sijui milioni ngapi za nini, tena mnasema mtapeleka cash wafanyie nini? (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashauri angalau wangesema kila kijiji kije na proposal kulingana na mazingira yake, kwa bajeti ya milioni 50 mtafanya nini? Mfano kijijini unasema sisi tunataka tuimarishe kilimo, tuna vijana hapa wanasoma mambo ya ugani kwenye vyuo vya kilimo, fedha hizi zikija sisi tutanunua maksai na plau. Kijana akirudi kutoka masomoni badala ya kulia anatafuta kazi tunamkabidhi plau halafu yule ng’ombe wa maksai anakuwa ni wa kijiji, unampa eneo anaendelea kulima pale organic food halafu ninyi mnatafuta soko la kuuza hizi organic food nje ya nchi kwa sababu zina soko sana kuliko hivi vyakula vya mbolea. Nyie mmeng’ang’ana na viwanda wakati mtaji hamna! Ooh sijui General tyre itarudi, Mbeya ZZK, nimechoka hata kuiulizia mpaka leo imebaki kuwa ghala tu la pombe ndugu zangu. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnasimama hapa mnasema tumenunua ndege (Bombadier), nataka niulize ni nani aliyepanga nauli za ndege hii kwa sababu highlight ya nauli wametoa. Sasa hizo Bombardier highlight ya nauli eti kwenda Mwanza Sh.160,000, kwenda Mbeya Sh. 305,000, kuja Dodoma Sh.3 00,000, hivi Mwanza na Dodoma mbali wapi au mnataka kumfurahisha ngosha? Tena huyu anatakiwa kutumbuliwa! Huwezi kusema nauli ya kwenda Mwanza ni Sh.160,000 ambako ni kilometa elfu moja na zaidi halafu kwenda Mbeya ambako ni kilometa 800 unasema Sh. 300,000…
MWENYEKITI: Malizia Mheshimiwa Mbilinyi muda wako umekwisha.
MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Ni inayounganika, nimetoka kuongea na Waziri Mkuu pale, sasa hivi kuna disaster diaspora. Serikali mmetoa tamko kwamba watu wote wa diaspora wenye passport za nje ambao wamejenga nyumba hapa zinataifishwa. Hii kauli imetolewa na Waziri wa Ardhi, Mheshimiwa Lukuvi and this is very bad na nimeongea na Waziri Mkuu, lakini naongea hapa….
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbilinyi muda wako umekwisha.