Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017

Hon. Lameck Okambo Airo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017

MHE. LAMECK O. AIRO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia kama ifuatavyo: Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa kuwa na aina nyingi za matunda. Ninaishauri Serikali kama bado wataruhusiwa wafanyabiashara kuingiza powder ya kuchanganya na maji na kutoa juice, hapo itafanya wawekezaji wa viwanda vya kutengeneza juice kushindwa kuwekeza, kwa sababu kijiko kimoja cha powder kinachanganya lita tano za maji na kutoa juice.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kuchangia kuhusu kiwanda cha maziwa Utegi; kiwanda hiki kilibinafsishwa kwa mwekezaji, lakini ameshindwa kwani mwekezaji huyo ameng‟oa mashine zote na majengo kubaki magofu. Ushauri wangu kwa Serikali ni kuchukua kile kiwanda na kumkabidhi mwekezaji mwingine ili wananchi zaidi ya 500 waliokuwa wakipata ajira kwenye kiwanda hicho waweze kupata ajira, hicho kiwanda kina eneo la hekta 10,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huo ndiyo mchango wangu.