Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia hoja ya bajeti ya Wizara iliyoko mbele yetu.

Awali ya yote ninataka kuipongeza na kuishukuru Wizara, Mheshimiwa Waziri na timu yako ya Naibu Mawaziri, Naibu Waziri Gekul wakati akiwa Naibu wako na ndugu yangu Mheshimiwa Ulega ambao wamefanya ziara katika Wilaya yetu na kutatua changamoto zilizokuwa zinatukabili, nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndugu yangu Mheshimiwa Ulega ulivyokuja lile ulilolifanya limeleta matumaini makubwa kwa Wana-Mkinga, lakini limeibua mahitaji makubwa sana, tunashukuru wa engine ya boti ile kwa kikundi kile cha ushirika, lakini sasa kuna vikundi kwenye mwambao ule karibu 12 mahitaji ya engine za boti zile kwa ajili ya uvuvi ni makubwa, nitawasilisha Wizarani kwenu kwa maandishi majina ya vikundi vile tunaomba mtusaidie. (Makofi)

Lakini Mheshimiwa Waziri tulifika Wizarani kwako na Madiwani wawili kuzungumzia changamoto ya mnada kwenye mpaka wetu wa Horohoro, nakushukuru sana, mma- act kwa haraka tumefanya jitihada sasa za kuanzisha mnada ule, naomba mwaka wa bajeti huu utakapoanza tukamilishe yale yaliyobaki ili mnada ule uweze kuanza, tuweze kupata mafanikio. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nijielekeze kwenye eneo la ufugaji wa samaki; ninaiona jitihada inayofanyika hasa hasa kwenye upande wa uzalishaji wa vifaranga, nawapongeza, lakini ninaamini bado tungeweza kufanya vizuri zaidi hasa kwenye ukanda wa Pwani tumeusahau, aidha tumeusahau au tunaogopa gharama za kuwekeza kwenye eneo hili. Ndugu zangu samaki wanaoliwa duniani zaidi ya asilimia 50 wanatokana na samaki wanaofugwa. Kwa hiyo, hatuwezi sisi kuacha kuwekeza kwenye eneo hilo, hatuwezi kuuacha uchumi mkubwa kiasi hicho, kuna kipindi nilisema hapa hivi wenzetu Afrika ya Kusini Western Cape na Eastern Cape wamewezaje kwamba eneo hili la ufugaji wa samaki linawabeba? Kwa nini tusiende kujifunza kule? Hivi kwa nini sisi leo hii tuzidiwe na Zambia kwenye kuzalisha na kuuza samaki? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miaka michache iliyopita tulikuwa tunazungumza na Katibu Mkuu Dkt. Tamatamah tukiona ni jinsi gani ambavyo Wazambia wale wamekwenda kupata fedha kutoka African Development Bank wameanzisha mradi mkubwa wa ufugaji wa samaki na sasa umeanza kutoa matokeo. Kwa nini sisi tusifanya hivyo? Lakini Wizara kwa nini msichukue initiative? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali hii imetoa fursa kwa Halmashauri kuwa na miradi ya kimkakati, watu wengi wanaenda kuwekeza kwenye stand na vitu vya namna hiyo, kwa nini ninyi Wizara msiichukue hii initiative, msichukue opportunity hii, mkatuma wataalam wenu kwenye Wilaya zile zinazopakana na hahari mkasema tunataka kutengeneza pilot district hata tano tu bila kuisahau Mkinga, mkaenda mkafanya study, mkafanya visibility study, tukaja na Mkakati Wilaya hizo badala ya kuwekeza kwenye stand waende wakawekeze kwenye ufugaji wa samaki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mkiweza kufanya hivyo mtaibua ufugaji wa samaki kwenye maeneo haya na shughuli za kiuchumi zitakuwa. Ninawaomba bajeti hii ikipita tumeni wataalam wenu Mkinga, waje tukae, tutengeneze visibililty study, tuweze kufuga samaki kwenye mwambao ule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. (Makofi)