Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. DKT. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi na mimi niweze kuchangia hoja ambayo iko mbele yetu. Kwanza naunga mkono hoja hii kwa asilimia 100. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya yote, natoa shukrani zangu sana kwa Mwenyezi Mungu kuweza kutupa neema yake ya uhai tukasimama leo hapa katika kazi zetu. Pili, nitoe pongezi nyingi sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na jitihada zake. Anafanya kazi kubwa sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo la Tanzania ikiwa ni pamoja na wasaidizi wake. Sijapata nafasi ya kuchangia hoja ya Waziri Mkuu lakini nitumie fursa hii kumpongeza sana kwa usaidizi wake kwa Mheshimiwa Rais pamoja na watendaji wakiwemo Mawaziri wa Ofisi yake ya Waziri Mkuu na Naibu Mawaziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tunampongeza sana Mheshimiwa Waziri Jafo. Mimi ni Mjumbe wa Kamati na nadhani katika Kamati ambayo imepata bahati kubwa ni Kamati yetu kutokana na kufanya kazi na Mheshimiwa Jafo pamoja na Naibu wake. Tunapata ushirikiano mkubwa sana katika Kamati yetu na kila hoja ambayo Kamati imekuwa iki-raise Mheshimiwa Jafo na wasaizidi wake walikuwa wanaifanyia kazi vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kamati yetu sisi tuna bahati nyingine kwamba Wabunge wengi na tofauti walikuwa wakihudhuria wakati tunapitia mafungu ya mkoa. Tulichokuwa tukikiona ni kwamba Wabunge wengi wakija pale wanakuwa pamoja na Wakuu wa Mikoa yaani ile agenda inakuwa ni moja kwamba sisi sasa tunakuwa hatuna namna. Mara nyingine hata wale Wabunge wao wanatoa clarity katika hoja mbalimbali ambazo sisi Kamati tunakuwa tumezi-raise.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimelisema hili ili tuone kwamba inapotokea hoja mtu inamuuma, inam-burn wakati yeye ni mmoja wa Wabunge katika Bunge letu na alikuwa kama linamuuma kweli kulikuwa kuna ratiba imetolewa publicly kila mtu anajua kwamba wengi walikuwa wanakuja na kuona kama kutakuwa kuna hoja basi hoja ile inazungumzwa pale na inatolewa maelezo na kama kulikuwa kuna issue ya kuchukuliwa, Mheshimiwa Jafo na wasaidizi wake hata pamoja na Wakurugenzi walikuwa wanachukua. Kwa hivyo, hizi hoja ambazo ziko petty, nadhani hazina msingi, tusichukue resource ya muda sana kwa ajili ya …

T A A R I F A

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Saada kuna taarifa, Mheshimiwa Mwakajoka.

MHE. DKT. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumpa taarifa Mheshimiwa anayezungumza. Hiki anachokizungumza tayari umeshakitolea maamuzi lakini pia ambacho nataka kukizungumza ni kwamba si kila Mbunge analazimika kwenda kwenye Kamati na Mbunge ambaye hajaenda kwenye Kamati pia ana mamlaka ya kuzungumza ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kitendo cha kusema kwamba angekuja kwenye Kamati ili aweze kupata ufafanuzi wakati ana nafasi kubwa ya kutoa hoja ndani ya Bunge anakuwa anamkosea Mheshimiwa Mbunge ambaye ametoa hoja za namna hiyo.

Kwa hiyo, nafikiri aendelee kuchangia tu mchango wake lakini asiseme tu kwamba angekuja kwenye Kamati, hiyo siyo hoja kabisa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwakajoka, jambo ulilolizungumza si kati ya taarifa mtu anazoweza kupewa. Unatumia Kanuni tofauti kama kuna jambo alilolisema ambalo hukubaliani.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tusikilizane ili tujue namna ya kwenda vizuri. Hapa haizungumziwi hoja ya Mbunge mmoja, Wabunge waliochangia ni wengi na wameonesha kwamba kwenye maeneo yao wana hoja ambazo wangependa zisikilizwe.

Mheshimiwa Saada anachofanya ni kuwakumbusha wajibu wetu. Kama una jambo ambalo ungetaka liingie huko kwa Mheshimiwa Jafo sasa hivi ulitakiwa kuwa umeshafanya huko. Hapa tunajadili sawa lakini hapa ni kwa ujumla lakini kila Mbunge ambaye ana hoja mahsusi alishaenda huko, ndiyo utaratibu. (Makofi)

MHE. DKT. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitunzie muda wangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi anayoifanya na kuna msemo wa Kiingereza unasema: “Life is not about duration, it is about donation”. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba mtu kadri unavyoishi, unaweza ukaishi miaka 5, 100, hakuna kitu ambacho wewe utakumbukwa nacho kama hujaleta mabadiliko chanya katika jamii ambayo wewe unaishi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo, Mheshimiwa Rais ameongoza katika kipindi cha miaka minne lakini donation yake katika maendeleo ya nchi hii ni kubwa mno. Nataka nilizungumze hili kwa sababu hata kule Zanzibar sasa hivi tuna Magufuli effect kwamba hata utendaji wa kazi umebadilika. Kwa hiyo, life is not about duration, tunaweza tukakaa Bungeni miaka mitano lakini kama hujaleta mabadiliko yoyote hata katika Bunge yaani umekuwepo wewe tu kama Mbunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona impact kubwa katika kipindi cha miaka minne katika maeneo mengi; huduma za jamii, afya, elimu, maji na hata kwenye financial infrastructures. Kwenye hili nampongeza sana Mheshimiwa Jafo kwa ubunifu ule wa kuwapa Wakurugenzi wetu mamlaka ya kununua Point of Sales (POS) umeleta impact kubwa kwamba hata wao sasa hivi wanajua wajibu wao katika masuala haya ya financial resources. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye hili nataka nimsisitize Mheshimiwa Waziri ahakikishe kwamba sasa hata Wakuu wetu wa Mikoa wanakuwa na ubunifu mkubwa zaidi wa vyanzo vya mapato. Maana masuala ya kusema kwamba fedha hazijapelekwa kutoka Hazina au zimechelewa isiwe ndiyo kikwazo cha kutotekeleza wajibu wao katika mikoa. Kwa sababu wao ndiyo wasimamizi wa mikoa lakini wajue wao ndiyo wasimamizi wa uchumi na maeneo ya mikoa husika, hata kama performance ya mkoa itakuwa ndogo, wanaowajibika ni wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ile kusema fedha hazijaletwa, kwa sababu hata fedha kukusanywa kwake kunategemea sana msingi wa nchi, eneo au tunasema regional intergration na hata uchumi mkubwa wa dunia. Kwa hiyo, ukiwa na excuse kwamba fedha hazijapelekwa it’s simply kwa sababu kunakuwa na effect tu ya dunia au region imetokea ambayo nchi tunakuwa hatuna control nayo.

Nataka kusisitiza kwamba Wakuu wetu wa Mikoa wawe wabunifu na hili nali-echo jambo ambalo tumelizungumza katika Kamati, wawe wabunifu wa kuleta maendeleo ya uchumi katika maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo nataka kulisema, katika mipango yetu ya maendeleo kuna vipengele vile vya mikoa wana components zile za afya na mara nyingi fedha zake tumezi-peg kutoka nje. Hata hivyo, tunajua kwa hili janga la Corona zile fedha it’s likely kwamba zinaweza zikapungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu wachangiaji wa fedha zile ambazo ziko katika mfumo wa basket fund ni wale bilateral donors ambao wengi wameathiriwa na maradhi haya ya Covid 19. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumesikia mwongozo na mikakati ambayo Waziri wa Fedha siku ya Jumatatu aliutoa vizuri lakini tuone kwamba afya ni jambo la msingi. Kwa maana hiyo ni lazima tuweke mkakati mahsusi ili activities zile ambazo tumezipanga kutokana na fedha zile zinazotokana na bilateral development partners zinatekelezwa kwa fedha zetu. Nina maana kwamba tujiweke tayari kuhakikisha kwamba tunaweza kutekeleza zile activities ambazo tumezipanga hususan kwenye sehemu ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu mwaka jana tulibadilisha sheria, zile asilimia 10 za mikopo ilikuwa hakuna walemavu ilikuwa ni wanawake na vijana lakini tulibadilisha ili tui-include component ya walemavu. Hata hivyo, wakati tunapitia bajeti za mikoa na progress they have made katika mwaka 2019/2020 tumeona kwamba fedha zinazokwenda kwa walemavu zimekuwa na changamoto. Changamoto kubwa ni kujitokeza kwa walemavu kuchukua mikopo na kufanya biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo, tunasisitiza kwamba hili jambo tuliangalie tena ili watu wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu tunaweza kuwa- accommodate vipi, aidha, wao wenyewe wasimame au tuweke misingi ambayo wale ambao hawako katika mahitaji maalum, wanawa-accommodate wale wenye mahitaji maalum kuona hii mikopo inakwenda vizuri kama vile ambavyo tumetarajia. Hili nadhani tulitafakari zaidi kuona kwamba vipi tutaweza kuwa-accommodate vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la nne, kuna vikundi vimejiendeleza vizuri sana. Nilikuwa nikiongea na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi the other day, kuna kikundi ambacho kimekuwa model kimetoka Mwanza katika eneo lake, wamefanya kazi nzuri sana. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri tunasisitiza tena, hebu tuangalie ile model ambayo wao wameifanya tuweze kuona wanawake na vijana wengine wanaiga ule mfano kupata uzalishaji zaidi na hivyo kuleta tija ili mifuko yetu iwe endelevu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pendekezo kwa Wabunge wenzangu wa Chama cha Mapinduzi ambao tunakwenda kugombea, hivi vikundi vinazalisha na wanatutegemea sisi sana. Kwa hiyo, zile harakati zetu wakati wa uchaguzi tuone kwamba zile tenda tunatoa kwa vile vikundi waweze kufaidika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, otherwise nakushukuru sana kwa wakati wako na ninaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)