Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, moja kwa moja nitakwenda ku-stress kwenye suala la utalii Southern circuit (Ukanda wa Kusini) naona mkazo bado kabisa. Wakati Mheshimiwa Waziri anazungumzia mafanikio ya watalii milioni 1.5 kwa mwaka jana waliotembelea Tanzania ningependa aniambie katika hao milioni 1.5 ni watalii wangapi walikwenda kwenye ukanda wa Kusini ikiwemo Kitulo, Ruaha, Katavi, Selous na hata Mbeya kama Mbeya tuna maeneo kama Lake Ngozi, Lake Kisiba, tuna Matema beach, tuna Ngonga beach yote hayo ni maeneo ya vivutio vya watalii kwenye eneo lile la Southern circuit. Kwa hiyo, nilitaka kujua kwamba katika 1.5 million ni wangapi walikwenda kutembelea kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuipongeza Wizara kwa ile branding ya “Tanzania unforgettable” it is a super thing. Nilivyoiona tu ile kitu nikasema sasa Dkt. Kigwangala yuko kazini lakini take it international; CNN, BBC na kwenye platform zingine za Kimataifa na wewe mwenyewe pia brother safari nenda Mamtoni, nenda Ulaya, nenda Marekani ukajue watalii wanataka nini ili uje uwaandalie hayo mazingira huko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenda wewe mwenyewe tu kutalii Serengeti, kwenda wapi haisaidii kuvutia watalii wa KImataifa ni sisi tu ambao tunakuwa na Instagram na maeneo mengine. Kwa hiyo brother utoke, uende Ulaya, uende Marekani ukajue watalii wanataka wanataka nini halafu sasa hii Tanzania unforgettable itakuwa imekaa sawa sawa na siyo ile channel yetu ya TBC ambayo tumeianzisha kutangaza utalii ambayo badala ya kutangaza utalii unakuta wanaonyesha miradi iliyofadhiliwa na TANAPA ya ujenzi wa vyoo na madarasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hiyo inasaidia vipi katika kutangaza utalii tunasema wkamba tumeanzisha ile channel kwa ajili ya kutangaza utalii ile inasaidia vipi kuonyesha kwamba TANAPA wako pale? Au unaonyesha madaktari wa wanyama wanachoma Tembo sindano. Kuna watu ni waoga hawapendi kuona hata vidonda vya wanyama ukiwaonyesha vile unawaogopesaha hata kwenda tena kutalii kwahiyo tuonyesheni vitu vizuri, tuonyesheni wanyama, tuonyesheni Ngorongoro, tuonyesheni Serengeti kupitia hii Tanzania unforgettable na siyo vinginevyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu tozo kwenye biashara; nitangaze interest kidogo, kwenye biashara za hoteli kama alivyoongea Mheshimiwa Lucy Uwenya jana tozo zimekuwa nyingi sana, unakaa mtu anapiga hodi mimi ni idara fulani nataka tozo, huyu anapiga hodi hatuwezi kwenda. Na tena ilitakiwa hoteli hizi mpya zinazoanza muwape nao kama miaka mitatu au at least miaka miwili ya task hizi tozo ili wakue kibiashara na hoteli zikikaa standard wakikua kibiashara huduma zikikaa sawasawa hao watalii mnaowavutia kuja watakuwa na sehemu sasa nzuri za kufikia, sehemu nzuri za kulala na si vinginevyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sana kwa sababu Mheshimiwa Waziri Mkuu jana amesema kwamba hizi tozo zitaondolewa naomba niiombe Serikali iondoe hizi tozo haraka sana kwa sababu matozo haya yamejazana katika biashara, sio tu biashara za hoteli hata biashara nyingine tofauti tozo zimezidi saba nchi hii ndio maana biashara hazikui, tuondoe tozo katika hizi biashara watu waajiri wakishaajiri hata wale wafanyakazi wanalipa kodi income task, wanalipa nini nayo ni njia nyingine ya kulipa kodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hizi kampuni au hizi biashara zinanunua bidhaa mbalimbali zinalipa kodi. Brother Mheshimiwa Dkt. Kigwangala concentrate kwenye kazi kwa sababu vitu vingine sometime unakuwa kama unaenda off step unavunja bodi halafu Mheshimiwa Rais siku mbili baadaye anakuja anairudisha vitu kama vile havitakiwi inakuwa ni kama political movies. Nakujua una potential yaani probably katika watu wanaokujua katika hili jengo na uwezo wako na potential wako mimi niko kwa kule tulikotoka forget about political issues, zile petty issues za politics, concentrate kwenye kutuongezea watalii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi kama Malaysia kwa mwaka wana watalii 25 milioni brother yaani wana watalii wengi kuliko population. Population ni 20 milioni lakini wanakuwa wana wataalii kwa mwaka 25 milioni ukiuliza vivutio hawana. Kuna siku nilikwenda Malaysia nikwauliza vivutio vyenu ni nini wakasema tuna maghorofa sijui ghorofa gani limejengwa kwa vyuma, tuna daraja gani, tuna beach na vyakula yaani mpaka vyakula wameviweka kama sehemu ya kivutio cha watalii. Sisi tuna madude yote haya kuanzia Ngorongoro, kuanzia Serengeti, kuanzia sijui Ruaha, kuanzia wapi kwa kweli tulitakiwa tuwe na watalii hata angalau milioni 10,15 kwa uwezo wetu wa kujitangaza, ahsante sana. (Makofi)