Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

Hon. Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Wizara ya Kilimo kwa kazi nzuri sana, wanayoifanya ya kusimamia na kutekeleza majukumu waliyopewa.

Mheshimiwa Spika, Zao la mahindi, halijapewa kipaumbele licha ya kuwa Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mikubwa minne inayozalisha mahindi kwa wingi sana na zao hili bado halijawekewa mkakati madhubuti wa soko na mbegu bora.

Mheshimiwa Spika, je, Wizara ina mpango gani wa kufanya utafiti wa mbegu bora ambazo zitaleta tija kwa mkulima kulingana na aina ya mbegu na udongo unaostahili kulimwa mahindi, na utafiti huo utachukua muda gani ili kuharakisha utekelezaji huo ili kuokoa nguvu za wakulima zinazopotea bure kwa uzalishaji usio na tija?

Mheshimiwa Spika, zao la tangawizi linalimwa sana katika Wilaya ya Songea Vijijini katika Halmashauri ya Madaba maeneo ya Mkongotema, Mahanje, Madaba, Wino na maeneo mengine. Tangawizi ni chakula, tangawizi ni dawa na imekuwa ikitumika sana katika mapishi mbalimbali. Je, Serikali ina mpango gani katika kuwekeza zao hili ambalo limekuwa linakuza uchumi katika nchi yetu ya Tanzania?

Mheshimiwa Spika, lakini, pia limekuwa likiuzwa ndani ya nchi yetu tu ilhali ziko nchi mbalimbali ambao wamekuwa wakitumia tangawizi kama chakula na dawa. Ninaomba Serikali ilete wataalamu katika maeneo yaliyotajwa hapo juu ili kuendelea kutoa elimu elekezi kwa wananchi. Ni imani yangu kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia sana kuongeza tija katika uzalishaji.

Mheshimiwa Spika, Masoko, soko la mahindi ni tatizo kubwa sana, ningependa Serikali itafute soko la uhakika la mahindi. Halikadhalika ninaomba Serikali itafute soko la tangawizi, mbaazi, mahindi na mazao mengine.

Mheshimiwa Spika, mwisho, Mawakala wa Pembejeo. Mawakala wa pembejeo hawajalipwa pesa zao kwa muda mrefu sana. Je, tatizo ni nini? Siku zote majibu ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha ni juu ya suala la uhakiki, je uhakiki huo utaisha lini? Mimi sioni kama mawakala wote walifanya udanganyifu kwa Serikali bali ninaamini kuwa kati yao wapo waliofanya vizuri. Sasa ni kwa nini hao waliofanya vizuri wasilipwe? Ninachelea kusema kuwa Serikali haiwatendei haki mawakala wa pembejeo, ninaomba mchango wangu Hansard.