Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

Hon. Riziki Saidi Lulida

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru na niunge mkono kwa asilimia 100 azimio hili la kuunga suala la Selous. Nafikiri utaniatambua uwepo wangu katika miaka yote niliyokaa katika Bunge hili nikiitambua Selous ni pori kubwa sana na ni kubwa na linahitaji mapato ambayo yatasaidia kuchangia Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, umenipa dakika tano kwangu nitazifanyia kazi. Pori la Selous kwa ukubwa wake lina eka za mraba 154,000 ni kubwa zaidi ya Serengeti, Serengeti ni 12,500 ni zaidi ya mara 12. Sasa leo TANAPA mnavyompatia nafasi ndogo katika Pori la Selous atapata wapi mapato, maana yake atakuwa amehifadhi?

Mheshimiwa Spika, ombi langu la kwanza Selous yote iwe ndani ya Hifadhi ya Mwalimu Nyerere kwa sababu za msingi. Tuna corridor ya Nyasa Selous ambayo ya Tanzania, ile corridor lazima iwe potential kwa ajili ya ile wanyama wanapotoka Mozambique wakija Tanzania itakuwa tayari migration ile inafanyiwa kazi, nani ataifanyia kazi hiyo migration? Leo TANAPA ina mapori au hifadhi 16, lakini zinazofanya kazi ni nne tu ambayo ni Serengeti, Kilimanjaro, Mikumi na kidogo Manyara, mmeiongezea pori hili kubwa, mapato yatapatikana wapi?

Mheshimiwa Spika, naomba usimvalishe shati, mvalishe na suruali anataka awe suti na kama itakuwa ni suti tunahakikisha pori zima la Selous liwe na hadhi moja tu na ninaomba hadhi hii itengezwe katika mazingira matatu; yenyewe Selous kwa vile ni kubwa itengenezwe zone ya Kusini, ya Mashariki na ya Magharibi ambayo ni Matambwe.

Mheshimiwa Spika, mkilifanya Pori la Selous mmelimega sehemu ndogo mtaleta migogoro mikubwa sana ambayo mtashindwa kuiendeleza. Ombi langu tembo ambao wanamalizwa ndani ya Pori la Selous ili kuwalinda na kuweza kuzaliana na nchi kuweza kupata mapato ningeomba Pori la Selous liwe lote moja tu hakuna kubagua, kumega na namwomba ujumbe huu ufike kwa Mheshimiwa Rais, ananitambua kama mimi Mama Selous na kama ni Mama Selous ni lazima Selous iwe neno moja tu Hifadhi ya Nyerere basi, masuala mengine italeta missunderstanding kwa vile kutakuwa na mapato yanataka kuingia ndani ya Selous, hapa kumechukua hifadhi ndogo pale Kibiti au Rufiji, ni eneo dogo sana bado kuna migogoro mikubwa ya wafugaji ambao wako ndani ya Selous, sasa tutaifanya iwe hifadhi hakuna mfugaji mle ndani wala ukulima mle ndani wala uchimbaji mle ndani, utaifanya nchi ipate mapato makubwa.

Mheshimiwa Spika, wewe ulikuwa Liwale unaijua Selous kwa undani wake. Leo Selous hii kuimegamega ni tayari unaitengenezea mazingira magumu na TANAPA mtawapa mzigo ambao watashindwa kuutengeneza. Leo TANAPA inaweza kuingiza mapato makubwa, lakini mapato yale kama hamjayatengenezea mazingira yake mazuri ina maana mtaifanya TANAPA iwe paralysed.

Mheshimiwa Spika, nataka niseme tena kusema Pori la Selous kuliweka katika hifadhi mmeiingizia uchumi nchi, ile migogoro tiliyokuwa tukizungumza kila siku na kelele tulizokuwa tunapiga sasa hivi tutakuwa tumemaliza kabisa. Matumaini yangu nendeni mkakae, mkajitathmini je, kwa nini tuchukue sehemu ndogo wakati Selous yote ile ni kubwa pori zima liingie katika hifadhi, msibague…

MHE. CHACHA R. MARWA: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Taarifa, endelea.

T A A R I F A

MHE. CHACHA R. MARWA: Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa mzungumzaji mama yangu, ukichukua Selous yote uifanye kuwa National Park utakuwa hujaisaidia, chukulia tu mathalani Serengeti National Park imezungukwa na game reserve, imezungukwa na WMA, hizi hapa ni zile ambazo zinasaidia pia wananchi ambao wanazunguka, ili kuona ya kwamba hii national..., kumbuka National Park huwezi kuwinda, huwezi kufanya chochote zaidi ya kupiga picha, lakini unapokuwa na game reserve pembeni unaruhusiwa kuwinda na kuvuna wanyama.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa nataka tu aone kwamba hili jambo lina umuhimu kwamba, sehemu iwe National Park na sehemu nyingine iwe game reserve kwa ajili ya kusaidia wananchi wanaozunguka. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Unaipokea hiyo taarifa, Mheshimiwa Riziki?

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, siipokei kwa vile hajitambui na hajui ninachokizungumzia ni nini, mimi nazungumzia mapato ya nchi, yeye anazungumzia ubinafsi na inabidi akalisome Pori la Selous ajue maana yake ni nini na potentiality ikoje. Na toka tumeanza uwindaji hakuna faida tunayoipata, tunataka Selous iwe ya mapato na maendeleo sio mabishano hapa tunataka kuijenga nchi, tunataka kumsaidia Rais, tunataka kumfanya Rais wetu aweze kutukuka ajue anachokifanya ni nini. Sio kutaka kuleta ushabiki wa kisiasa.

Mheshimiwa Spika, hapa mimi sizungumzi siasa, ninazungumzia uchumi wa nchi ambao utaifanya nchi yetu iweze kupaa na Rais vilevile anachokifanya wao ambao walikuwa wanapingana nae anataka kuiweka nchi ikae katika reform, hivyo sikubalianinae na ninaomba aje nimuekeleze ajue mimi Mama Selous naijua Selous kwa undani wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuzungumza hayo niiunge mkono hoja na ninasema tena ninawaunga mkono kwa vile leo TANAPA inapewa mzigo mkubwa sana. Sasa tutapompa Selous ambayo haina potential kama ilivyo kwa Kitulo, Kitulo imepewa katika hifadhi haina potential, Katavi iko katika hifadhi haina potential, Buruwando iko katoka hifadhi haina potential, Gombe iko katika hifadhi haina potential, haya tunakwenda maeneo mbalimbali ya hifadhi ambayo wamepewa hayana potential wanategemea maeneo manne tu na Selous kwa vile yana potential na Selous watalii wanaijua kama Selous ni eneo potential.

Mheshimiwa Spika, ni Serikali ya kusimama kuwahakikishia dude hili tunalifanyaje ili iingize mapato. Masuala ya ushabiki, siasa, hakuna, hapa tunataka uchumi ambao utakuwa endelevu na utamsaidia Rais Magufuli katika maendeleo yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hapo nawashukuruni sana. Ahsanteni sana. (Makofi)