Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo

Hon. Dr. Augustine Philip Mahiga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoka pongezi kwa Wenyeviti wa Kamati zote tatu ambazo leo zimetoa ripoti zao kwenye Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ningependa kutoa msisitizo kwa kutoa pongezi na shukrani kwa Kamati ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo ambayo ni ya muhimu sana katika utendaji kazi wa Kamati ya Katiba na Sheria kwanza kabisa Mwenyekiti ameonesha werevu na uadili wa hali ya juu kwa sababu yeye mwenyewe ni Mtaalamu wa Sheria lakini pia ameonesha uwezo wa uongozi wa kuwaleta karibu wanachama wake katika mijadala mbalimbali na kutoka Vyama vyote ambavyo ni wanachama wa Kamati hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijawahi kuona umoja na mshikamano katika mijadala yao kama niliyoshuhudia katika Kamati ya Katiba na Sheria chini ya Mwenyekiti huyu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimeshuhudia kwamba wanachama wa Kamati ile wana uelewa wa hali ya juu wa mahitaji ya nchi hii katika kuleta haki katika nchi hii. Haki ni moja ya huduma muhimu katika nchi kama vile tunavyozungumzia Maji, Afya, Elimu haki ni kitu muhimu na Kamati hii imeonesha umuhimu wa kuleta haki kwa watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Kamati hii imeonesha kwamba ni wasikivu kwa wadau mbalimbali siyo wao tu wanazungumza kama Kamati, siyo wao tu wanazungumza na sisi kama Wizara lakini wanakaribisha wadau mbalimbali kutoka Mashirika mbalimbali na hii inarutubisha demokrasia ambayo tunatakiwa kuwa nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nawashukuru Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria kwa usimamizi wao wa Miradi mbalimbali ambayo Wizara yangu imekuwa ikitekeleza hawazungumzi tu wanakwenda mpaka kuiona mimi nimeshiriki nao tumetembelea Mikoa ya Mbeya, Arusha, Manyara, Kigoma na kule wamehakikisha kwamba wanasimamia Miradi hii inatekelezwa kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wameleta mawazo ambayo teknolojia ya ujenzi ya sasa hivi imeleta mapinduzi makubwa katika ujenzi wa Mahakama zetu huko mikoani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nataka niwashukuru Mwenyekiti na Kamati kwa jinsi walivyosimamia Bajeti yetu katika Awamu hii ya Tano sijawahi kuona na nikilinganisha na Bajeti nyingine jinsi tulivyopewa pesa na jinsi pesa zilivyopangwa ili tuweze kufikia mwelekeo wa kufikisha haki karibu na wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwelekeo huu nina uhakika yale tuliyoyapata katika Awamu hii ya sasa haitachukua zaidi ya miaka mitano kukamilisha yote ambayo malengo Wizara yangu imeweka hasa katika kusogeza haki karibu na wananchi na kuboresha utumishi wa Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia natoa shukrani za pekee na hapa lazima nisisitize Mheshimiwa Rais ametuteulia Majaji wa Mahakama Kuu na Majaji wa Mahakama ya Rufani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uteuzi huu umeleta tofauti kubwa sana katika kusukuma maamuzi ya Mahakama na kuhakikisha kwamba mrundikano wa Mahakama, mrundikano katika Magereza unapungua na kama tutaendelea kupata ushirikiano wa namna hii na hasa katika raslimali watu nina uhakika kwamba malengo yetu yatafikia mahali pazuri na tutaweza kushona lazima ushone haki na demokrasia na katika mfumo huu tumefika mahali ambapo utawala bora kwa sura ya haki kwa Raia umejidhihirisha kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kutoa shukrani pia kwa kusaidia na kuunga mkono Taasisi zangu hasa RITA ambapo tumekwenda na ninyi katika Mkoa wa Iringa kushuhudia uandikishaji na utoaji wa Vyeti vya watoto chini ya miaka mitano na kuendelea kutoa Vyeti katika Mikoa mingine kwa namna ambayo haijawahi kutokea na tunafanya karibu na NIDA na katika zoezi hili lililokwisha sasa hivi RITA imeshiriki kikamilifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Wizara yangu pamoja na Taasisi na zake tutaendelea nimalize kwa kusema ahsanteni sana Wabunge wote kwa mchango wenu leo katika mijadala hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yote mliyoyasema, yote mliyochangia tutayatekeleza nina unga hoja iliyotolewa hapa ahsante sana. (Makofi)