Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kwa Uamuzi wake wa Kulifanya Bunge Kutekeleza kwa Vitendo Dhana na Bunge Mtandao (e-Parliament)

Hon. Dr. Jasmine Tiisekwa Bunga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Vyuo Vikuu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kwa Uamuzi wake wa Kulifanya Bunge Kutekeleza kwa Vitendo Dhana na Bunge Mtandao (e-Parliament)

MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu katika kumpongeza Mheshimiwa Spika kwa maamuzi mazuri ya kutekeleza ahadi yake ambayo binafsi nilifikiri labda tunaishia hivihivi bila ya tablets au bila ya kuwa na e-Parliament. Tunashukuru sana kwa sababu sasa katutoa kwenye analojia tunarudi sasa kuwa Wabunge wa kidigitali zaidi. Kama walivyozungumza wachangiaji wenzangu kwa kweli, tutaokoa pesa nyingi lakini pia itasaidia suala zima la utunzaji wa siri na katika kutunza kumbukumbu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa dhati kabisa nimpongeze Mheshimiwa Spika kwa uzalendo wake. Kama tulivyoona tumetumia wataalam wetu wa ndani. Watu wengi wanasema degree za Tanzania haziajiriki, hazina mshiko, jamani hawa ni watu ambao wamesomea utaalam nchini kwetu na ndiyo wanatumika. Kwa hiyo, kwa uzalendo huu tutaokoa pia pesa nyingi kwa ajili ya matengenezo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kweli, naungana kwa dhati kabisa na wenzangu kumshukuru sana Mheshimiwa Spika, nampa hongera sana kwa kazi nzuri ambayo anaendelea kuifanya. Ahsante. (Makofi)