Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Hon. Yussuf Kaiza Makame

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Chake Chake

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru awali ya yote kwanza nimshukuru Mwenyenzi Mungu, lakini pili niendelee kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Chake Chake kwa kuniamini, lakini tatu nikishukuru chama changu na niwashukuru pia wananchi wa Chake Chake kwa kuendelea kuyaheshimu maazimio na maagizo ya chama chao. (Makofi)
Baada shukrani hizo naomba sasa nianze kuchangia hoja, na nianze kwa kumnukuu Rais wa mwanzo wa Afrika ya Kusini Iliyohuru, Hayati Nelson Mandela aliwahi kusema; “education is the most powerful weapon which you can use to change the world.” Elimu ndio silaha pekee, taaluma ndio silaha pekee inayoweza ikatumika kuubadili ulimwengu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie kiriri hiki, nitumie nyumba hii kusema kwamba elimu ndio silaha pekee ya kuibadili Tanzania, si jambo linginge. Si Jeshi, si Polisi wala si kingine kitakachoweza kuibadili Tanzania isipokuwa tutumie elimu yetu, tu-invest kwenye elimu ndio itakayoweza kututoa hapa tulipo tukaenda tunapotaka. The best way ni kutumia elimu kwenda kwenye uchumi tunaoutaka wa viwanda, the best way ni kutumia elimu kwenda kwenye demokrasia halisi na mambo mengine yenye faida kwa Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la mikopo limezungumzwa na wazungumzaji wengi, wachangiaji wengi wamelizungumza suala hili kwa kina. Ila kwa sababu na mimi ni mdau katika suala hili la mikopo naomba nizungumze kwa mantiki ifuatayo; kwanza niwashukuru kama Serikali niwashukuru kwamba mmeianzishia sheria maalum, sheria mlitunga, Namba 9 ya mwaka 2004 ya kwamba isimamie Bodi ya Mikopo ambayo itawezesha kuwapa mikopo vijana wetu wa elimu ya juu, lakini sheria hii ikaeleza kwamba wanaopaswa kupewa mikopo ni wale tu wenye mahitaji ya kupewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, si kila Mtanzania kwamba anapaswa kupewa mikopo kwa mujibu wa sheria hii, ila practically ni vinginevyo. Wale watu waliosoma katika shule za kayumba wanakoseshwa mikopo na wanapewa watoto wa Mawaziri na watoto wengine wa vigogo. Kwa hiyo, niseme suala hili lina changamoto kubwa, kwanza ucheleweshaji wa mikopo ya wanafunzi, ni changamoto kubwa kwa Serikali na hii ndio inayosababisha migogoro baina ya Bodi ya Mikopo na wanafunzi na Wizara ya Elimu, ucheleweshaji wa mikopo ya wanafunzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, , lakini pili wanafunzi wasio na sifa, kupewa mikopo hii, lakini lingine Ofisi za Kanda zimefunguliwa kwenye suala la mikopo. Kuna Ofisi za Kanda katika Miji Mikubwa kama Mbeya, Arusha, Zanzibar, lakini ofisi hizi pengine kuna mtumishi mmoja tu ambaye hawezi kutimiza majukumu ya kikanda, Zanzibar akuna mtumishi na kuna Ofisi ya Kanda. Lakini wanafunzi wanaopata mikopo kutoka Bodi ya Bara au Bodi ya Muungano ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wanalazimika kusafiri kutoka Zanzibar kuja Bodi ya Mikopo Dar es salaam.
Mheshimwia Mwenyekiti, tulitengemea sisi ile ofisi ya Kanda iliyopo Zanzibar isaidie kutatua kero za wanafunzi wanaopata mikopo pale Zanzibar. Kwa hiyo, hii ni tatizo nini result ya changamoto hizi za wanafunzi, nini result yake, matokeo yake wanafunzi wanaandamana hovyo hovyo, baadaye mnaweka ma-red block kila mahali. Mfano leo tu, hatuhitaji hata kutoa historia leo tu wanafunzi wa natural science wa Chuo Kikuu cha Dodoma walitaka kuandamana kuja kudai fedha na hawajawahi kuingia darasani toka tarehe Mosi Aprili. Leo wanakuja kudai fedha, kutumia njia za kidemokrasia kwa sababu maandamano ni haki, mnawanyanyasa, mnaweka magari humo, tension barabarani, vitambaa vyekundu wanakuja hapa kuomba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni la mikopo mnawapelekea baada ya maandamano, kingine ni kuwafukuza wanafunzi. Wanaandamana mnawabandikizia kesi, huyu CHADEMA, huyu nani, huyu CUF jambo ambalo si la msingi kabisa, watu wanadai haki ya msingi kabisa. Lakini changamoto nyingine wanafunzi wanaenda wakijiuza, kwa sababu ya kukosa mikopo hii kwa wakati. Baadae mnaanza kudili watu wanaojiuza sijui huko Dar es Salaam wasiwepo na nini, ninyi hamjatimiza wajibu wenu Serikali ya CCM, tafadhalini timizeni wajibu wenu kwa wanafunzi hawa, tujenge Taifa letu kwa pamoja.
Mheshimwa Mwenyekiti, ushauri wangu, Serikali kupitia Wizara ya Elimu kwanza itimize wajibu wake wa kupeleka fedha kwa wakati, mpeleke fedha ili kuepuka changamoto hizi, lakini pia wanafunzi wanapoandamana kwa kudai haki na ninyi mkijua kwamba fedha hizi hamjawapa kwa wakati muwaache wadai haki zao kwa sababu wanaeleza hisia zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ni kwamba hili suala la Dkt. Suleiman alilolieleza Baraza la Mitihani. Kuna Baraza la Mitihani (NECTA), mimi nataka kulizungumzia kivingine kabisa, ni kwamba Baraza la Mitihani ndio linalopanga division au GPA. Miaka mingi tumekuwa tumekuwa tukitumia division, mwaka 2012 kukafeli wanafunzi wengi hasa kutoka Zanzibar ikaundwa tume na Waziri Mkuu iliyoongozwa na Profesa Sifuni Mchome na Wabunge humu akina Mwenyekiti Mbatia walikuwemo, Mkaja na mapendekezo waliyopendekeza kwenda kwenye GPA lakini sasa siku saba tarehe Mosi mlienda Waziri....
Kengele ya kwanza…