Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuunga hoja mkono na kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote kwa kazi nzuri inayoonekana. Hata hivyo, bado ningependa kushauri na kujua hatima ya uanzishaji wa Chuo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) maeneo ya Amani -Muheza. Majengo ambayo Mheshimiwa Waziri ameyaona yanazidi kuharibika bila kutumiwa, ningeshukuru kama suala hili litapewa umuhimu wa kipekee. Aidha, bado tunakumbushia suala la gari la wangonjwa, (Ambulance) ambapo katika Jimbo la Muheza hatuna kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la dawa ya nyoka kupewa bure kwa wananchi naomba lizingatiwe kwani bei ya dawa hizo ni ghali sana.