Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Hon. Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ubadhirifu katika miradi ya maji. Kwenye miradi ya maji kuna ubadhirifu mkubwa sana. Hii inasikitisha sana pale ambapo Serikali inatoa pesa na pesa zile haziendi kufanya kazi iliyokusudiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Litola kuna mradi wa maji wa zaidi ya shilingi milioni 200 lakini mradi ule haufanyi kazi una zaidi ya miaka mitatu. Kata ya Mkako kuna mradi wa shilingi milioni 718, mradi huu maji hayatoki lakini pesa asilimia karibu 90 imeshalipwa kwa mkandarasi. Sasa mimi nashindwa kuelewa hili jambo linakuwaje na wakati huo huo, katika utekelezaji huu huwa kunakuwa na Mhandishi Mshauri, Mhandishi Mshauri ambaye anashauri miradi kama hii hapa ambayo mwisho wa siku inagharimu pesa nyingi na haiwezi kutoa maji na kufikia malengo tunayokusudia amechukuliwa hatua gani? Naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa aseme katika miradi hii iliyofanyiwa ubadhirifu ni watu gani ambao wamechukuliwa hatua ili tuweze kujua vinginevyo Mheshimiwa Waziri nashindwa kukuelewa pale ambao upo hapo lakini pia hatusikii chochote kinafanyika kuhusiana na hawa watu waliofanya ubadhirifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri Mbarawa kwamba kuna dhambi ambayo hawezi kuikwepa hata ikawaje. Mkoa wa Ruvuma katika Kata nilizozitaja, Kata za Litola, Mkako, Nandembo ndoa za watu zimevunjika kwa sababu ya kukosa maji. Akina mama wanafuata maji umbali mrefu, kwa hiyo, kuna ndoa ambazo zimevunjika, Kata ya Litola ndoa tatu zimevunjika, Mheshimiwa Waziri atajibu. Kata ya Mkako ndoa tisa zimevunjika, wanawake wanafuata maji umbali mrefu. Kata ya Nandembo hali kadhalika ndoa nne zimevunjika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hawatendei haki Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma kwa sababu sasa wanaondoka kwenye hali ya kuwa na ndoa zao wanaanza kuwa ma-bachelor. Niombe sana utakapokuja unijibu. Naomba sana Mheshimiwa Waziri Mbarawa nisaidie katika hili kuhakikisha kwamba miradi hii niliyoitaja iliyogharimu pesa nyingi, nijue ni nini ambacho kimefanywa kwa sababu katika Mradi wa Mkako, shilingi milioni 718 zinaendelea tu mradi haufanyi kazi, umeacha tafrani katika maeneo husika. Naomba tafadhali sana sana sana, wanawake wa Mkoa wa Ruvuma tunakulilia ndoa zetu zinavunjika kwa sababu ya kufuata maji umbali mrefu, waume zetu wanakosa imani, tunashindwa kuwahudumia waume zetu, kwa hiyo, tunakosa sifa ya kuwa wanawake bora wa kuhudumia familia zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maneno haya, naunga mkono hoja, Mheshimiwa Waziri naomba ajibu kwa nini miradi hiiā€¦

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)