Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na taasisi zake kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, katika Nchi ya India kwa suala la usalama barabarani, wao ikifika saa tatu usiku huanza kuwakagua madereva wote ili kutambua kilevi kwa lengo la kuzuia vifo vingi vinavyotokana na ajali za barabarani wakati wa usiku. Kwa mfano huo wa Nchi ya India, naliomba Jeshi letu la Polisi liangalie uwezekano wa kuanzisha utaratibu huo wa ukaguzi wa kilevi kwa madereva wakati wa usiku ili kuzuia ajali nyakati za usiku ambazo nyingi zinasababisha vifo kutokana na ulevi wa madereva.

Mheshimiwa Spika, Madereva wa Serikali wadhibitiwe kwa kuendesha magari kwa kasi na kutoku-overtake sehemu za hatari.