Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Asha Mshimba Jecha

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha majengo ya vituo vya Polisi na nyumba za makazi kwa Askari wetu. Naomba Serikali kutukamilishia ujenzi wa Kituo cha Polisi Dunga ambacho kinahitaji kiasi cha shilingi milioni 50 kwa matengenezo ya ndani; kuweka sakafu, madirisha, milango, plasta ya ndani na nje, hard board na uzio.

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Polisi Makunduchi, nyumba za makazi ya Askari wa kawaida hali zake ni mbaya sana, mbovu. Tunaomba majengo hayo yajengwe upya.

Mheshimiwa Spika, naomba Maaskari wetu wapatiwe posho na stahili zao kwa wakati. Wapo Askari wameziomba posho hizo kwa kuandika barua, na katika ziara ya Mheshimiwa Waziri na Naibu pia, Askari wameziwasilisha changamoto hizo lakini hakuna hatua yoyote ya mabadiliko na hawajapatiwa hadi leo. Mbaya zaidi kuna Askari wameajiriwa mwisho kuliko wengine, tayari wamepatiwa posho hizi. Mfano, mwaka 2004 hawajapata posho lakini 2006 anapatiwa posho, wakati kazi yao ni moja, vyeo sawa na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, wapo Watanzania wengi hawajapatiwa Vitambulisho vya Taifa na wanashindwa kujitafutia fursa na kuzitumia kwa wakati stahiki. Basi tunaomba vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi vitumike katika kuzifikia fursa hizo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja. Ahsante.