Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana. Naomba nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kunipa uzima niweze kuchangia leo tena hapa kwenye hii hoja ya TAMISEMI. Kwanza, nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo, ni moja ya Mawaziri ambao wako very humble and mobile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi nikiwa ng’ambo ile, Mheshimiwa Jafo alitutembelea Wilaya ya Serengeti akaona jitihada zetu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Serengeti, Jafo hakusita akatuletea fedha na hospitali inaendelea vizuri. Nikushukuru sana kwa mwaka huu Mheshimiwa Jafo umetupa shilingi milioni 500, Mungu akubariki sana lakini pia naomba unifikishie salamu hizi kwa Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Biblia Zaburi ya 11:3 Biblia inasema,”Kama misingi ikiharibika, mwenye haki atafanya nini?” Hakuna ubishi kwamba nchi huko nyuma ilikokuwa inaenda ilikuwa inaenda kubaya kweli kweli. Upande wa kule ng’ambo walikuwa na nguvu sana kwa sababu kwa kweli mambo hayakuwa mazuri. Nakumbuka kabla sijawa Mbunge, nikiwa Diwani na wanasiasa wengi waliojifunzia upande wa kule kama mimi, hoja kubwa waliyokuwa wanaitumia ni ufisadi. Ufisadi ulikuwa ni tiketi ya wewe kuhakikisha unaing’oa CCM. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ndugu zangu tukubaliane ukweli, kwa mfumo ambao Mheshimiwa Rais Magufuli amekuja nao, kwanza kwa kuanzisha kitu kinaitwa Treasury Single Account ni mfumo bora ambao hakuna kiumbe yeyote anaweza ku-temper nao kirahisi. Unalipa kila mtu anaona; Serengeti wamelipa hiki, wamefanya hiki na kinakuwa evaluated. Kwa hiyo, namshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikiliza Mbunge mmoja ng’ambo ile anasema kwamba, decision making iliyofanywa na Chama cha Mapinduzi, chini ya Mwenyekiti, Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Magufuli kununua ndege kwamba ni maamuzi mabaya. Ngoja niwaambie, wakati wengine tukiwa nje ya Bunge hili kipindi kilichopita, waliokuwa wanaipinga Serikali kwa nini hakuna ndege za nchi, mmojawapo alikuwa Mheshimiwa Mch. Msigwa. Akasema nchi gani hii hatuna ndege! Alikuwa Mheshimiwa Mch. Msigwa huyu. Ndege zimenunuliwa anaanza kupiga kelele. Hawa watu vinyonga hawa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukikaa ukamsikiliza Mheshimiwa Mch. Msigwa, kila siku anaongelea uwanja wa Nduli, hivi uwanja wa Nduli uko Jimbo gani? Si Iringa? Anasema watengeneze uwanja wa Nduli. Sasa watapeleka ndege gani? Hawa ndege wanyama au! Ndege wa angani ndiyo wataenda kwenye uwanja wa Nduli! Si lazima tununue ndege ziende kule ili kuleta watalii watakaoenda Ruaha National Park. Watalii wataendaje Ruaha National Park bila ndege? Kwa hiyo, lazima tununue ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mtu anapinga Stieglers Gorge. Hivi jamani, si tumeona kila siku, sisi tunaijua hapa, si tunaelewa! Mheshimiwa Rais amesema tunataka umeme rahisi. Umeme rahisi ni wa maji. Labda ile Kambi wangesema sisi Kambi ya Upinzani tumefanya utafiti, tumegundua umeme rahisi ni wa gesi. Hizo tafiti mlizofanya ziko wapi Mheshimiwa Mch. Msigwa? Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefanya utafiti wa vyanzo vyote vya umeme, imegundua umeme rahisi ni wa maji. Leo utatokea wapi? Ni Stieglers Gorge, yaani unapinga na hiyo? Aaaah mura! (Makofi/Kicheko/ Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie Serikali ya Chama cha Mapinduzi ni Serikali sikivu. Kweli kabisa ni sikivu. Issue ya kikokotoo, ni kweli ilipita sheria hapa, tulipitisha Wabunge wote, si na wewe!

MBUNGE FULANI: Eeh!

MHE MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ilipitishwa hapa. Mheshimiwa Rais alivyo msikivu, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi akasikiliza wafanyakazi akasema, hakuna, hii rudisha huko. Sasa hiyo nayo unapinga tena kwamba eti ni maamuzi mabaya! Aaah mura! (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikiliza mwingine anasema, Serikali ya Chama cha Mapinduzi waongo, waliahidi mwaka jana shilingi bilioni 29 za maboma, ziko wapi? He, unaishi wapi wewe? Mheshimiwa Dkt. Magufuli alishatoa hela, yaani huko madarasa yanafunikwa, madarasa yanakamilishwa na hakuna watoto watakaoshindwa kwenda shule. (Makofi/Kicheko/Vigelegele)