Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mikakati gani kuanzisha Mfuko wa Wazee utakaowezesha wazee wasiokuwa kwenye ajira rasmi kujiajiri kwenye shughuli za uzalishaji mali? Wapo wazee wenye nguvu na uwezo wa kuunda vikundi kwa ajili ya uzalishaji na shughuli za ujasiriamali tatizo kubwa hawana mtaji. Umri wa ujana unaishia miaka 45, wazee kuanzia miaka 46 kuendelea ambao hawana pensheni wanaishi kwa tabu sana vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imetenga baadhi ya shule za msingi kwenye Halmashauri ya Wilaya na Miji kwa ajili ya kusajili watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu). Nini mkakati wa Serikali kuwezesha miundombinu ya shule hizi kuwa rafiki kwa ajili ya watoto hawa walemavu wa aina mbalimbali? Nini mpango wa Serikali kupeleka walimu wenye ujuzi na taaluma ya kufundisha watoto hawa wenye mahitaji maalum ili waweze kunufaika na elimu kama wanafunzi wengine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la vijana kutokuwa na ajira linaendelea kila siku na kila mwaka vijana wanamaliza vyuo vikuu, vyuo vya kati katika fani mbalimbali. Ni vijana wachache sana wanapata ajira Serikalini na kwenye sekta binafsi. Nini mkakati wa Serikali kuwezesha vijana wengi kujiajiri kwa kuwapatia mitaji na vifaa/mashine za kufanyia kazi za ujasiriamali kwenye viwanda vidogo vidogo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kilimo ni sekta inayoajiri watu wengi ni maeneo yapi na wapi yametengwa katika Mikoa mbalimbali ili kuwezesha vijana kujishughulisha na uzalishaji mashambani?