Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana na kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kusimama nikiwa upande huu wa pili, naomba nichukue nafasi hii kumshuruku Mungu kwa neema aliyonipa kuwa upande huu. Ni bahati sana unajua kuwa Mbunge wa pande zote wakati kama huu nimekuwa upande wa kule ng’ambo na leo niko hapa, I can taste the difference. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kitu nimejifunza na nitaomba nikiseme, kazi ya Bunge au kazi ya Mbunge ni kuikosoa, kuishauri na kuisimamia Serikali. Lakini nimegundua kumbe kipindi nikiwa ng’ambo ile nilikuwa nakosoa tu nilikuwa sishauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nitakosoa, nitashauri na naomba nianze kwa kunukuu maneno aliyoyasema Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1969 alisema hivi; “Taifa lisilokubali kutaabika kwa maendeleo yake lenyewe, bila shaka Taifa hilo litataabika kwa maendeleo ya mataifa mengine, anasema maendeleo ni mtoto wa taabu.” (Makofi)

Naomba nirudie hawajasikia vizuri; “Taifa lisilokubali kutaabika kwa maendeleo yake lenyewe, bila shaka Taifa hilo litataabika kwa maendeleo ya mataifa mengine, maendeleo ni mtoto wa taabu.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kuendelea kwa kutegemea donors, kama ingelikuwa mataifa yanaendelea kwa kutegemea donors tungeona kwa China, tungeona kwa Amerika na mataifa mengine. Lakini ni mataifa ambayo yaliamua kutumia rasilimali zao wenyewe na leo wako hapo walipo wanasaidia watu wengine na nampenda sana Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli yeye hataki tujiite sisi maskini na kweli sisi siyo masikini, Tanzania siyo masikini. (Makofi/ Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuna maeneo naomba nishauri eneo la kwanza…

T A A R I F A

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa leo niongelee mwenendo wa thamani ya shilingi. Ukiangalia kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ambayo mimi pia ni Mjumbe wa Kamati thamani ya shilingi inashuka na kuna mapendekezo yametolewa nini kifanyike ili ku- stabilize shilingi yetu. Sasa kama nilivyosema leo nitakosoa kwamba ni kweli tumeendelea kushuka shilingi yetu imeendelea kushuka, lakini nini kifanyike ili shilingi yetu iendelee kuwa stable.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kwanza, lazima tukubali kama Bunge kuisimamia Serikali ipeleke fedha za kutosha kwenye kilimo. Kwenye kilimo wenzangu wameshauri kwenye yale mazao ya kimkakati kwa mfano tumbaku, korosho na mazao mengine ambayo yanatuingizia fedha za kigeni lazima tuhakikishe tunawekeza huko, sasa huo ndio ushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili, nina kiatu hapa, hebu kiangalie vizuri kwanza, hiki hapo, kiangalie vizuri hicho kiatu, hiki kiatu ukikiangalia utadhani kimetoka Ulaya, kinatengenezwa hapa Dodoma.

MBUNGE FULANI: Nyoosha juu tukione. (Makofi)

MHE. MARWA R. CHACHA: …hapa Dodoma, hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima tu-discourage importation ya vitu tunavyoweza kuvitengeneza wenyewe. Leo tuna ng’ombe kila kona, tuna ngozi ya kutosha, lazima Serikali ichukue hatua ikiwezekana ya kuondoa kodi kabisa kwenye mashine za uchakataji wa ngozi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda kwa huyu mtu ambaye anatengeneza hivi viatu, yuko hapo karibu na Chuo cha Mipango, ni mjasiriamali mdogo tu, lakini unaweza ukaangalia ukadhani kimetoka Ulaya. Sasa tutawawezeshe tuwasaidie watu wetu wazalishe vitu vyetu, soko la ndani ni kubwa. Badala ya kuagiza nje tuzalishe vya kutosha na tuuze nje shilingi yetu itakuwa imara kwelikweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ushauri mwingine ni kwenye mafuta. Tupige kodi kubwa kwenye mafuta ya kutoka nje ili watu wetu walime alizeti, walime michikichi, tuzalishe mafuta yetu wenyewe. Haiwezekani shilingi yetu ikawa stable kama mafuta tunatoa nje, haiwezekani. Hivi ni kweli tumeshindwa kulima alizeti? Tumeshindwa kuzalisha mafuta ya alizeti? Haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima tuchukue mkakati wa makusudi na mimi namshukuru sana Rais John Pombe Magufuli, alisema kama hamlimi sitoi chakula, umesikia watu wanalia njaa saa hizi? Wamenyooka, watu wanalima, watu wanalima, hakuna cha dezo kila mtu afanye kazi fursa zipo. Kwa hiyo lazima tukubali kuzalisha zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine, tuwasaidie wachimbaji wadogowadogo wa madini. Nichukue hatua hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Madini, Mheshimiwa Doto Biteko ameanza vizuri. Nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kukubali kukaa na wachimbaji wadogo wadogo na wachimbaji wakubwa, ni hatua nzuri, tumuunge mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuwasaidie wakandarasi wa ndani kwa sababu hapa ndipo pia tunalipa fedha nyingi za kigeni kwenda nje. Leo tungekuwa tumewezesha watu wetu wakandarasi wa ndani kufanya miradi yetu fedha zinabaki humu ndani, zinazunguka humuhumu. Kwa hiyo, tuendelee kuwawezesha wakandarasi wa ndani. Nimshukuru pia Mheshimiwa Rais Magufuli kwa sababu ndiye mwanzilishi wa kusaidia wale wakandarasi wa ndani waliojenga Daraja la Mbutu kule Igunga, na sasa hivi wako kule wanatengeneza barabara, wanaenda vizuri na wametengeneza Daraja la Mto Mara ambalo liko mpakani kati ya Jimbo la Serengeti na Jimbo la Tarime na Mheshimiwa Heche anafahamu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Chacha.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia, naomba nimalizie. Nilikuwa naomba nishauri kwenye eneo lingine ni TARURA, tumeunda chombo hiki TARURA ili kusaidia barabara za vijijini, tunaomba Serikali ilete chanzo kingine cha kui-finance TARURA ili ifanye kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda nashukuru, lakini niseme nilimsikia mtu mmoja anasemasema pale ni Mchungaji, sijui mchungaji? Are you a Pastor or Poster?