Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Spika, takribani asilimia 90 ya Watanzania hutumia nishati ya kuni na mkaa kwa matumizi ya nyumbani, hali hii huleta uharibifu mkubwa wa misitu nchini. Inasemekana kwa wastani hekta 400,000 hupotea kila mwaka. Ni kwa nini Wizara hii isishirikiane na Wizara ya Nishati ili kuja na mikakati mahsusi ya kutumia nishati mbadala nje ya mazao ya misitu?

Mheshimiwa Spika, TFS imekuwa ikitoa leseni za kuvuna bidhaa za misitu ya kwenye ardhi ya kijiji bila kushauriana na mamlaka husika ya kijiji. TFS imekuwa ikikusanya tozo (collecting revenues) kwenye bidhaa za misitu zilizovunwa kinyume cha sheria, ikiwa ni pamoja na mkaa na mbao na kujiongezea mapato. Pia kuna malalamiko kuwa TFS haina ushirikiano mzuri na jamii zinazojishughulisha na hifadhi za misitu (community foresty management) na kuwachukulia kama washindani, hali hii pia hujitokeza kwa kukwamisha harakati za CSOs na NGOs.

Mheshimiwa Spika, ripoti ya NARFOMA inaonesha kuna jumla ya hekta milioni 48 za misitu wakati idadi ya watu ni trakribani milioni 50. Kwa hiyo bila usimamizi sahihi wa misitu tutaangamia. Kuna haja ya kuwa na mipango sahihi ya kuangalia, kwa mfano matumizi ya biomass energy, mikaa bado ni changamoto. Mashaka haya yanabidi kushughulikiwa ikiambatana na marekebisho ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji katika misitu inapaswa kukuzwa kwa kuzingatia vigezo vya utunzaji/uvunaji endelevu (sustainable harvesting) ili ku-address economic, environmental and social issues.

Mheshimiwa Spika, kuna alternatives nyingi nchini za vyanzo vya umeme ambavyo havina madhara makubwa sana katika ekolojia ya maeneo husika pamoja na jamii inayoitegemea, sasa basi, ni kwa nini Serikali inang’ang’ania kutumia Stieglers Gauge ilhali itasababisha madhara makubwa kwa rasilimali maji, maliasili na shughuli za kiuchumi? Rufiji Basin Hydropower Master Plan imeainisha maeneo mengine yenye uwezo wa kutoa umeme kama Kihansi, Ruhudji, Mnyera na Kilombero.

Mheshimiwa Spika, ukataji wa miti zaidi ya 1,430 km2 ni janga kubwa kwa Taifa, hasa kwa maeneo ya Kusini (Selous), Rufiji Delta na kadhalika katika maandalizi ya mradi huu wa Stieglers.