Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mkoa wa Tabora watumishi wa sekta ya afya ni wachache kwenye maeneo yote na hili ni tatizo la muda mrefu, wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma ni wengi. Vituo vya afya vina wahudumu watatu mpaka wanne tu na wanafanya kazi usiku na mchana. Zahanati nyingi zina nurse mmoja na mganga mmoja tu. Ikitokea akapata dharura hakuna huduma na maeneo mengine wanatoa huduma wasio na taaluma za afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itoe kipaumbele kwa Mkoa wa Tabora kupelekewa watumishi wa afya kwani uhaba huo, hata takwimu za kitaifa zinaonyesha miaka zaidi ya minne iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kaliua hakuna Hospitali ya Wilaya; tumeanza kujenga OPD kwa kutumia fedha za ndani na nguvu za wananchi. Tumejenga jengo la ghorofa moja kubwa lenye vyumba muhimu vyote na sasa tuko kwenye hatua za mwisho. Serikali iko tayari kutoa fedha kusaidia kuongeza nguvu kwenye jengo hili ili likamilike na Hospitali ya Wilaya ianze?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kaliua lenye kata 13 lina vituo vya afya viwili tu. Serikali mwaka wa jana ilileta barua Wilayani ya kutaka kila kata mbili ziandae maeneo ya kujenga vituo vya afya, maeneo hayo yameshaandaliwa. Ni lini ujenzi wa vituo hivyo utaanza maana bajeti hii Waziri hajasoma lolote kuhusu mpango huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la bima ya afya limehamasishwa na wananchi wengi wamejiunga, tatizo kubwa ni pale wanapokwenda hospitali, vituo vya afya, zahanati wanakosa dawa. Kwa nini Mfuko wa Bima ya Afya hauboreshwi sambamba na uwepo wa dawa zakutosha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la sekta ya afya kutaka kuwa watoto under five years, wajawazito na wazee zaidi ya miaka 60 kupata huduma bure halijatekelezwa katika maeneo mengi sana. Wazee wakienda vituoni bila pesa hawapati huduma. Pamoja na Waziri/Serikali kutoa kauli hapa Bungeni mara ngapi mbona bado ni tatizo? Leo Mheshimiwa Waziri atoe kauli ambayo itatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado wanawake wengi na watoto wanapoteza maisha kwa kukosa huduma ya mama na mtoto. Kuwepo kwa zahanati chache, vituo vichache na kukosekana kwa mobile clinic ni chanzo cha kupoteza wanawake wengi na watoto bila hatia. Wilaya yangu ya Kaliua hakuna kabisa mobile clinic na hakuna gari la kupeleka chanjo kwenye maeneo ambayo hakuna vituo. Serikali inaokoaje maisha ya akina mama wa Kaliua kwa kupeleka gari moja tu katika Wilaya ya Kaliua na kwa kuzingatia kwamba jiografia ya eneo la Kaliua ni kubwa na mapori mengi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo tatizo kubwa sana kwa wananchi kununua dawa zinazotembezwa barabarani na makampuni mbalimbali na kutibu magonjwa bila kufanyiwa vipimo wala kujua vipimo sahihi na mbaya zaidi wanakuwa hawana ujuzi wowote ni kama njugu. Je, Serikali inaliona tatizo hili? Bahati mbaya kuna nyingine ni za kunywa/kumeza. Kwa nini Serikali inaruhusu biashara huria ya dawa kwenye mabasi, vilabuni, njiani na barabarani? Afya ya wananchi inalindwaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hizi Hospitali za Mission kama vile KCMC ambazo Serikali inawekeza nguvu ili wananchi wapate huduma kama hospitali ya Serikali, je, sera ya afya kwa makundi yale muhimu kupata huduma bora inatekelezwa kwenye hospitali hizi? Wapo watoto waliopewa rufaa kwenda KCMC kupata matibabu walipofika kule wakaambiwa KCMC si hospitali ya Serikali hivyo huduma zote ni kulipia. Serikali itoe ufafanuzi kwa hospitali zote za aina hiyo.