Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.

Hon. Daniel Edward Mtuka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.

MHE. DANIEL E. MTUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii na mimi nitoe mchango wangu kwenye Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa moja kwenye barabara zangu za hadhi ya mkoa, kwa maana ya jimboni kwangu Manyoni Mashariki. Ubora wa barabara hizi si wa kuridhisha, ninaomba sana Wizara husika, nadhani watu wa TANROADS Mkoa huwa hawaendi kusimamia ujenzi wa barabara hizi, kwanza upana hauko sawasawa, tuta linanyanyuliwa katikati, magari makubwa ya mizigo hayawezi kupishana na mpaka sasa hivi magari mawili yameanguka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia madaraja; ukienda kwenye daraja lile la Mto wa Sanza, nilipita juzi pale! Nakuomba Mheshimiwa Waziri siku moja tupange safari twende kule ukaangalie tulinganishe BOQ na kitu ambacho kipo kule kwenye lile daraja lenye mita mia moja, ni refu. Nimekuta kitu cha ajabu sana kule, nondo milimita sita inajenga daraja! Milimita sita! Hii ni hujuma ya ajabu sana. Naomba tuangalie ubora katika ujenzi wa barabara na hasa katika usimamizi wa hizi barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa moja upande wa ujenzi wa kituo kinachoitwa One Stop Inspection Station pale Muhalala; hivi vituo ni vitatu katika hii central corridor, moja ni kule Muhalala. Sasa tatizo ni kwamba wale wananchi hawajalipwa fidia. Mwaka wa tatu sasa hawafanyi shughuli zao za kimaendeleo, hawalimi, hawajengi na ardhi imechukuliwa, lakini hawalipwi fidia. Naomba Waziri akijumuisha atoe majibu, lini watalipwa fidia watu hawa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa moja kwenye reli ya kati. Naomba niungane na Wabunge wenzangu, reli hii ni ya gharama kubwa sana standard gauge, nadhani katika historia ya nchi hii hatujawahi kuingia mradi mkubwa wenye thamani kubwa kama huu. Naomba tutafute mkandarasiā€¦
MWENYEKITI: Ahsante.