Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Hon. Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru pia kwa kunipa nafasi ya kuchangia nadhani niende moja kwa moja kwenye hoja na hasa tunapojadili mapendekezo haya ya mpango. Kwa sababu kauli mbinu yetu ya miaka mitano hii ya Mpango wa Maendeleo tunasema kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu. Nita-base kidogo kwenye viwanda zaidi sasa nimejaribu kupitia Mpango na Taarifa ya Kamati niwapongeze sana watu wa Kamati ya Bajeti kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wameifanya ya kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kwa upande wangu nilikuwa nataka kujikita kwenye viwanda kama nilivyosema na hasa kwa kuangalia kwenye Ilani yetu ya chama tumesema kwamba tunataka kutengeneza ajira na ajira nyingi zaidi ziko vijijini na viwanda siku zote tumekuwa tunasema hapa kaulimbiu yetu ni kuhakikisha tunakuwa na viwanda vitakavyotumia mazao ya kilimo, mazao ya mifugo uvuvi kwenye madini na sehemu nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa sababu ya athari za UVIKO nimejaribu kuwa nafuatilia trend ya biashara inavyoenda kwenye dunia kwa sababu sisi tuko na wenzetu na tunafanya kazi na mataifa mengine duniani na hasa kwa sasa tunaona kwa sababu ya effect ya Amerika kujifungia na kufanya nini tumeona kwamba gharama kubwa za usafirishaji wa bidhaa nyingi duniani zimepanda kwa sababu demand and supply imekuwa kubwa sana hasa kwa USA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukirejea hata kwa upande wetu bidhaa nyingi ambazo tunatoa nje. Kwa mfano kusafirisha Kontena moja ya bidhaa ya 20 ft kutoka China, ilikuwa ni dollar 2100, dollar 2000 mpaka dollar 1900 as we speak juzi nadhani Jumatatu nilikuwa najaribu kufuatilia baadhi ya sehemu sasa hivi kontena moja ya 20 ft imefika dollar 4900 kuitoa China kuileta hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye 40 ft inaenda dola 9800 mpaka dola 10000. Sasa zote hizi zina effect kwenye upande mmoja hasa kwenye upande wa biashara hasa viwanda wanapokuwa wanaagiza malighafi za kuleta hapa zinakuja kuleta shida sana kwa sababu cost of production itaongezeka kwa sababu ya ile transportation ambayo ipo hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tukiangalia kwenye upande wa kilimo tumekuwa na kelele nyingi sana za mbolea hapa wote mnaelewa lakini mbolea haikupanda kwa sababu ya Tanzania imepanda kwa sababu ya hii hali ambayo inaendelea na hasa usafirishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nikawa nawaza kitu kimoja wakati tunaongelea ule mpango wa kutengeneza eneo huru la biashara la Afrika niliongelea kwamba wenzetu ambao tupo nao kwenye sehemu moja hii ya biashara wapo tayari kwenye GMO products. GMO products ambazo zinatumika kwenye viwanda na baadhi ya sehemu nyingi hasa mazao kama pamba na vitu vingine wenzetu wameshatoka kwenye teknolojia ya kawaida huko wapo kwenye teknolojia ya mbele zaidi. Kwa sababu wote tunajua advantage ya zile product, leo tunasema kwamba tunaingia kwenye ukame tuna- expect mvua zinaweza zikawa zimepungua, lakini unapokuwa kwenye upungufu wa mvua ukawa na products zile za GMO mbegu zile kinachosaidia ni nini, kwamba ile mbegu inaweza ikavumilia ukame, lakini mbegu ile haihitaji mbolea nyingi kama leo ambavyo tunahangaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nasema kwamba katika Mpango Serikali ijaribu kuangalia pia kwa sababu tunaongelea jambo la 2022 kwenda 2023 tuone hii hali ya sasa hivi kwenye bajeti ya sasa hivi tumeshaiacha, lakini tunapoenda mbele tujaribu kuona kama Serikali can we adopt this technology? Maana hii teknolojia itatusaidia kwanza kuwa competitive na pia kuweza kuhimili hali ya hewa kama hii ambayo inabadilika badilika kwa sababu hatujui baada ya hapa kitakachotokea nini. Kwa hiyo, niliomba hili jambo tuliangalie ili tusiathiri viwanda vyetu hivi ambavyo vina-deal na mazao ya kilimo na ambavyo vimeajiri watu wengi na watanzania wengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika Mpango kuna jambo moja nilikuwa naliangalia tumewekeza fedha nyingi sana kwenye miradi mingi ambayo inaendelea. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa pesa ambayo imepatikana kuna pesa nyingi zimeenda kwenye miradi ya maji na nyingine zinaendelea kutoka kwenye bajeti yetu, lakini nimekuwa najaribu kuangalia trend kila ukiangalia milioni 500, milioni 400, milioni 500, milioni 400 fedha ambazo zinapelekwa kwenye miradi ya maji, nikawa najiuliza katika best engineering practice hakuna kitu ambacho unakifanya bila kuwa na plan ya kuki- maintain baada ya pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana kwenye upande wa barabara tumekuwa tunatenga pesa kupitia road fund lami hizi hizi ambazo tumezijenga kwa hela nyingi bado ipo pesa ya kuendelea kuzi- maintain nikajiuliza what is the plan hasa kuhusu miradi ya maji mikubwa ambayo tumeifanya kwenye maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema haya kwa sababu unajenga kituo cha afya cha milioni 250 yupo Daktari pale na wapo watu wanaendelea kuki-maintain kile kituo. Ukijenga madarasa Walimu wapo pale wanaendelea kuya- maintain, lakini miradi ya maji ambayo inatumia pesa nyingi za Watanzania wote ni mashahidi hakuna watu ambao ni technical or qualified people ambao wana technical knowledge wanaosimamia ile miradi ya maji. Zaidi ya kuunda ma-group tunasema ma-group ya watumiaji wa maji, vyama vya watumiaji wa maji unakuta pale ni Mwenyekiti wa Kijiji na Mtendaji wa Kijiji ndiyo wanaosimamia, technically hawajui kile kitu, kinachokuja kujitokeza ni nini miradi hii itakuja kututoa jasho baada ya miaka mitano baada ya miaka sita miradi itakufa tutaanza kuwekeza pesa nyingine tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa sababu tumejenga vyuo vingi sana vya VETA kila anayesimama hapa anaomba chuo cha VETA kwenye Jimbo lake, kila anayesimama anaomba chuo cha VETA kwenye Jimbo lake tunao vijana wale, wale vijana gharama yao siyo kubwa, wanaweza wakafanya kazi katika mazingira yale ya chini kwa sababu ndiyo kada ya chini kabisa kwenye ufundi ambayo inaweza ikafanya zile kazi.

Sasa tuombe Serikali mjikite kwenye kufikiria ajira za vijana hawa ambao tunawatengeneza kupitia vyuo vyetu vya VETA tuwapeleke vijijini wakakae kule wao ndiyo wawe mafundi wa ngazi ya chini wa kusaidia miradi ile maji ambao tunaweka hela nyingi wailinde na waweze kui-maintain. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimezunguka kwenye Jimbo langu kuna baadhi ya sehemu vilichimbwa visima, pesa nyingi imetumika baada ya miaka mitatu kisima kimekauka. Lakini kama una mtu ambaye is a technical qualified person yule mtu ange-inspect kwamba hapa kuna shida akajaribu kujulisha hata kama maji yanapungua usiunguze hata ile pampu vile visima havifanyiwi service, pampu ile ukiichimbia kule chini mpaka siku ikiharibika ndiyo unakuja kuangalia baada ya muda inaharibika na ina-cost hela nyingi. Pampu ambayo inakuja ku-cost shilingi milioni mbili, milioni tatu, milioni nne, tungeweza kui-maintain kwa shilingi laki moja, laki mbili tukaitoa tukaipeleka sehemu tukasafisha tukairudisha. Lakini yote hiyo ni lazima kuwe na a best plan ya kuhakikisha vitu hivi tunavyovifanya pesa tunazowekeza ziwe na watu wa kuzifuatilia na kuzisimamia na by the way ni sehemu ya kutengeneza ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi yangu yalikuwa hayo nilitaka tuone mpango mzuri kwenye hasa upande wa maji wakusimamia hii miradi mizuri ambayo tunaifanya baadae miradi hii isije ikatutokea puani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayo naomba kuunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)