Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Dr. Paulina Daniel Nahato

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi na mimi kuchangia katika Wizara hii. Napenda sana kuipongeza Wizara hii chini ya Waziri pamoja na mdogo wangu Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayofanya. Kwa sababu nina dakika tano mimi naomba nichangie katika eneo la utangazaji.

Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu suala la utangazaji au habari; ufikishaji habari ni haki ya kila na hata katika ilani yetu ya chama pia tumejipambanua kwamba kila mwananchi ana haki ya kupata habari sahihi. Sasa nitaenda moja kwa moja kusema kwamba katika channel zetu za tv upatikanaji wa habari bado hautoshelezi na usikivu wa channel hasa channel ya TBC ni limited na kama tunavyofahamu katika maeneo ya pembezoni sehemu kama Ngorongoro ambayo ni eneo kubwa, lakini upatikanaji wa habari kwa sehemu hii kwa kweli ni hafifu na maeneo kama Namanga, maeneo kama Longido na Bukobwa zile sehemu ambazo ziko pembezoni wale wananchi hawapati habari.

Mheshimiwa Spika, habari ni muhimu sana, kwa mfano kama hotuba za Rais ni muhimu kila mwananchi akaisikia. Kwa hiyo, mimi naishauri Serikali iweze kuangalia hili kwa sababu habari ni muhimu katika kulinda nchi yetu, jambo lolote la hatari litakapotokea ni vyombo vya habari ndivyo vitakavyotumika kusambaza habari na mambo kama ujenzi wa uzalendo, mambo kama utamaduni wetu vyote hufikiwa kwa habari. Kwa hiyo usikivu wa channel ambao kwa mgano tuna channel yetu ya TBC ambayo ni asilimia 63 na ni channel ambayo ni ya Taifa tunaomba hii iwekewe mkazo iweze kufikia watu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo la pili kwa haraka niende kusema kwamba naiomba Wizara iangalie suala la wasanii wetu waweze kutengeneza tamthilia. Kwa sasa hivi tumejikita zaidi katika sinema zetu na unakuta hazifurahishi kwa sababu nyingi sinema ni fupi na kwa sababu hata wale wanaocheza sinema wengi wanajitegemea, hawana pesa za kutosha mtu ukiangalia filamu unajua itaishiaje.

Kwa hiyo hata hupati mvuto wowote unajua tu hii sinema imeanza climax yake itaishia hivi. Kwa hiyo haupati ile hamu ya kuangalia. Lakini filamu kama Isidingo na filamu zingine za nje ni nzuri kwa sababu zinakupa hata mtu umechoka kusikiliza.

Kwa hiyo, nilikuwa naomba Wizara iangalie kutengeneza tamthilia ndefu kama Isidingo, lakini iwe inaakisi tamaduni zetu, lugha yetu na itaweza kujenga Taifa kwa ubora na watu watakuwa na hamu ya kuiangalia mara kwa mara kwa sababu mtu hatajua inaishiaje na hivyo basi pia tutatengeneza uchumi na itaweza kuwajenga vijana kuwa na weledi wa kuweza kutengeneza filamu zenye ubora kuliko sasa hivi ambazo tunaangalia nyingi zimejielekeza katika mapenzi na mambo fulani fulani ambayo ni kwa ajili tu ya kupata kipato kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine naomba kusisitiza juu ya mambo ya channel ya utalii. Channel ya utalii bado haijakaa vizuri, coverage yake bado haitoshi utalii wetu unatakiwa utangazwe sana waandishi wa habari nimepata habari walipata semina kutoka Tanzania nzima, lakini unakuta wanapokwenda kutengeneza filamu za utalii pesa haitoshi, wanakwenda katika mbuga za wanyama au sehemu mbalimbali wanakaa siku tatu. Siku tatu utatengeneza filamu gani? Haiwezekani na yote hayo ni kwa sababu ya pesa, ili utengeneze filamu nzuri inatakiwa muda na vitu vyote vile vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa kifupi siwezi nikasema lakini naomba channel hii ya utalii hata watalii wenyewe wanapokuja wakati mwingine kutokana na usikivu kuwa hafifu wanaulizia channel za utalii, mtu hajui nakumbuka mimi nilipokuwa Marekani mtalii mmoja alikuja akasema mimi nimengalia channel, lakini sijaona mlima Kilimanjaro je, wewe umeuona? Nikamwambia nimewahi kuuona, akanikumbatia, akaniambia daktari nafurahi nimemshika mtu ambaye amepanda Mlima Kilimanjaro. Lakini Mlima Kilimanjaro ungetengenezewa channel nzuri ungeweza kuleta watalii kwa wingi zaidi. (Makofi)

Kwa hiyo naomba kusisitiza kwamba hii safari channel na channel zingine ziwepo na zitengewe pesa ya kutosha ili ziwe na coverage nzuri yaku-capture utalii wetu na uweze kusambaa dunia nzima na iwe ni channel ambayo ni imara zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine la mwisho sasa labda kwa ajili ya muda haraka napenda kusemea juu ya…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Paulina Nahato.

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono hoja. (Makofi)