Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, naomba awali ya yote nianze kwanza kwa kutoa shukrani zangu za dhati sana kwako kwa fursa hii ambayo umenipatia, lakini nitoe pia shukrani kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango mizuri sana na mikubwa mliyotupatia ya fikra na mawazo chanya kwa ajili ya kuweza kupeleka mbele sekta zetu hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kwa namna ya kipekee nimshukuru sana Waziri wangu, Mheshimiwa Mashimba Ndaki na Makatibu Wakuu wote wawili pamoja na wataalam wetu na Wakuu wa Taasisi na Idara mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa shukrani hizi nitoe pongezi nyingi pia kwa Wabunge kwa namna ambavyo wametupa michango yenye kujenga sana, wakiongozwa na wewe mwenyewe ambaye kiasili ni mfugaji, tunakushukuru sana na tuna hakika kwamba michango yenu hii tunakwenda kuifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa uchache wa muda ninaomba nijielekeze katika kujibu hoja kadhaa za Waheshimiwa Wabunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nitaanza na upande wa mifugo na naomba niseme juu ya mipango yetu ya kibajeti kama ambavyo inasomeka katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wabunge walio wengi wameeleza wazi juu ya kutokuridhika kwao kwa namna ambavyo nchi yetu ina mifugo mingi sana, lakini bahati mbaya sana mifugo hii kutokuwa na mchango mkubwa kwenye pato la Taifa na katika pato la mwananchi mmoja mmoja.

Mheshimiwa Spika, Serikali tumeliona jambo hili, jambo hili linatufanya sisi kama wauzaji wa mifugo tusifanikiwe sana kwa maana suppliers na demand (mahitaji) ni makubwa sana. Kwa hiyo sisi Watanzania wote tunaowajibu wa kuhakikisha tunalichukua kama fursa jambo hili. Na nini ambacho tumejipanga nacho ili sisi Watanzania tuweze kuitumia vyema hii advantage ya kuwa ni suppliers wa mifugo tena duniani.

Mheshimiwa Spika, moja ya jambo kubwa linalotusumbua kwa kipindi kirefu, mifugo haina insurance, ni perishable good, jambo hili limetufanya hata bankers wasiwe na appetite ya kuweza kuingiza pesa katika shughuli za mifugo. Leo hii tunakwenda kwa mfano katika Eid, wakati wa Eid biashara nyingi sana ya mifugo inafanyika, jamii ya Kituruki peke yake inanunua na kuchinja ng’ombe wasiopungua 15,000, jamii moja tu hiyo, lakini utatazama namna biashara ile inavyokwenda.

Mheshimiwa Spika, ukiitazama biashara ile inavyokwenda yule mnunuzi anataka awe supplied wale ng’ombe na akishakuwa supplied wale ng’ombe ndiyo sasa baada ya wiki moja hadi mbili aweze kulipa. Jambo hili linawafanya watu wetu wasifanikiwe kwa sababu hawana cash na wanapokwenda benki hawawezi kupata hii pesa kwa sababu tu mifugo as a perishable good, haikubaliki katika kupewa pesa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumefika hatma ya jambo hilo, NIC wanaenda sasa kutupa uhakika wa kuwa na bima ya mifugo ambayo itawafanya wafugaji wetu wawe na uhakika wa kwenda kukopesha katika miaka minne hii TADB Benki yetu ya Kilimo imeweza kupata application za mikopo ya shilingi bilioni 85, mikopo pekee waliyoitoa katika miaka minne hii ni shilingi bilioni 26. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama kweli tunataka twende mbele ni lazima tutoke mahala huko, lakini kama haitoshi moja ya mkakati ambao wameusoma Waziri hapa ni kuhakikisha kwamba tunaboresha kosafu zetu, kwa nini kosafu zetu, tunahitaji kuwa na quality ya ng’ombe, tunahitaji kuwa na quantity ya uhakika, tunahitaji kuwa na constant supply ya ng’ombe. Kwa sababu leo tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais na ninampongeza sana Mheshimiwa Waziri alishiriki kikao cha Mheshimiwa Rais pale Ikulu, Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, watu wapo tayari kununua ng’ombe wetu, lakini leo hii mtu mmoja akiambiwa apeleke constant supply ya tani saba kila mwezi hapa tutatafutana, ni kwa sababu ya constrain ya kuwa na kosafu na mipangilio yetu haijakaa sawasawa. Wizara imejipanga vyema katika risala hii utaona tumeweka pesa zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya kufanya massive artificial insemination, tunakwenda katika Halmashauri zote zenye mifugo na kuhakikisha kwamba hatuishii kuwapandisha tu, lakini kuna gharama kubwa ya kuwaweka kwenye heat. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wale ng’ombe jambo linalowasabisha wafugaji wengi washindwe ni kukaweka kwenye heat, tunataka tuwapeleke kwenye heat synchronization kwa makundi, tutakuja Kongwa, tutakwenda Kiteto, tutakwenda Monduli, tutakwenda Longido, tutakwenda kote kwa wafugaji na kule kwa Dkt. Chaya alipopasema ambapo ni Manyoni. Tukiyafanya haya ya kupata massive artificial insemination tutapata kosafu zetu na baada ya muda tutaanza ku-realize juu ya kuwa na ng’ombe walio bora. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, biashara ya unenepeshaji ng’ombe ni biashara ya uhakika sana, ninawaomba Waheshimiwa Wabunge wakati tunaendelea kuhamasisha jambo hili sisi wenyewe pia vilevile tuwe ni mfano mzuri sana, ni utajiri wa wazi ambao mimi ningeomba sana Wabunge wengi tuingie, leo unamnunua ng’ombe ana kilo 150 ambaye huyu ukimchinja carcass weight yake ni nusu maana yake kilo 75, ukimpeleka sokoni hakubaliki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini ng’ombe huyo ukienda katika project ya kunenepesha maana yake ni siku 90; kwa hii breed yetu ni nusu kilo kwa kila siku, lakini kwa breed ya boran ni kilo moja kwa kila siku, kwa hivyo huyu ukimpa siku zako 90, huyu ng’ombe anakwenda kuwa na kilo zaidi ya 150 kwa hiyo atakuwa na kilo takribani 240 mpaka kilo 300 ambayo akipata carcass weight anapata kilo 150 hadi 200 na ukimpeleka sokoni anauzika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeeleza hili, ili kuwapa Waheshimiwa Wabunge matumaini na namna ambavyo Wizara yetu ilivyojipanga hiyo ni sambamba na kwenda kutatua kero kubwa inayotusumbua kwa muda mrefu ya gharama za flight na Serikali kupitia Wizara yetu ya Ujenzi na Uchukuzi, umeona tumejipanga vyema eneo hili katika kuhakikisha kwamba…

(Hapa kengele ya kwanza ililia)

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nasikia kengele hiyo.

SPIKA: Bado dakika tano

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi imeandaa kununua ndege mwaka huu ndege ya cargo itakayobeba a straight destination, kwa hiyo hapa tutachukua nyama zetu zitakwenda Jeddah, zitakwenda Oman, zitakwenda wapi moja kwa moja, kwa hivyo hii ni fursa kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia vilevile tulikuwa na tatizo kubwa la delay pale katika bandari yetu ya Dar es Salaam kwa sababu mizigo yetu hii ikienda inakaa kwa muda mrefu. Wizara ya Ujenzi imejitahidi, naomba tusikate tamaa, tunawaombeni kwa heshima kubwa tupitishieni bajeti yetu, mipango ya Serikali tuliyonayo ni mikubwa ya kuhakikisha sekta hii inakuwa ili kusudi sasa iweze kuchangia vyema katika pato la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie sasa kwa upande wa uvuvi; uchumi wa blue; uchumi wa blue umesemwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika risala ya Mheshimiwa Rais ameeleza vizuri sana, tutanunua meli, meli nne Zanzibar, meli nne Bara na katika mwaka huu 2021/2022 tunaanza nalo jambo hili.

Waheshimiwa Wabunge wengi wa Zanzibar walitaka kujua jambo hili linafanyika Bara tu au linafanyika na Zanzibar tunafanya kwote kuwili hapa bara tunanua meli mbili na kule Zanzibar tunanunua meli mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tena tuna pesa za kutosha za kuhamasisha ufugaji wa samaki katika Ukanda wa Pwani, tunazaidi ya shilingi bilioni 15 zinazokwenda kufanya kazi hii, hii ni pamoja na mwani, hii ni pamoja na kaa unenepeshaji, hii ni pamoja na majongoo bahari, hii ni pamoja na kazi zingine zote zitakazowasaidia vijana sio tu Bara tunakwenda mpaka Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge tunawaombeni sana mjipange katika mkao ule wa vyama vya ushirika na vikundi vya vijana hawa ili tuweze kuitumia vyema hii fursa. Nataka niwahahakishie kwamba jambo hili lipo tayari na tumejipanga nalo vyema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama haitoshi katika kuhakikisha kwamba tunaongeza productivity kule baharini, tunacho kitu tunaita FADS yaani Fish Aggregative Devices, hii tunakwenda kuweka kule katika bahari, tunazo hizi ni takribani tisini zitaenea katika ukanda wote ule wa Pwani, hii nia yake ni kuwavuta wale samaki.

Mheshimiwa Spika, mmoja katika Waheshimiwa hapa, Mheshimiwa Asya Mwadini alisema kwamba samaki sasa wanakosa maeneo ya kuzaliana. Tumeliona jambo hili na sayansi yake ndiyo tunakwenda kuweka zile fish aggregative devices kuanzia Moa mpaka kule Mtambaswala zitaenea hizi, hizi nia yake nikuongeza mazalia ya samaki, hilo jambo tayari tunalo tupitishieni huu mpango ili tuhakikishe kwamba tunakwenda kuyafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama haitoshi, jambo lingine zuri tunalokwenda kulifanya ni kuanzisha vichanja vya samaki; ukanda wote huo utapata vichanja vya kukaushia dagaa wetu, hatutaki kuona dagaa wanaoza, hatutaki kuona samaki wanaoza, hii ni rasilimali ya Taifa letu, tunataka tuone watu wanaendelea ku-export na nimewasikia Wabunge wengi wanazungumzia juu suala la kuhakikisha kwamba wale foreigners wanaokuja kununua, sisi wenyewe ndiyo tuwawezeshe watu wetu wazawa ili waweze kununua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kwa sababu ya muda naomba nimalizie kwa kuwaeleza na kuwapa matumaini Waheshimiwa Wabunge wote, Serikali yetu imejipanga vyema katika hii blue economy na pesa za kununua meli zimeandaliwa, zipo tayari kwa maana mradi huo upo, ujenzi wa bandari hili lipo tayari pia vilevile na tunashirikiana vyema sana, kwa maana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Bara, lakini na Wizara yetu kwa upande wa kule Tanzania Visiwani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa kwa umuhimu, katika kujibu changamoto inayowapata wafugaji wengi tunakuja na teknolojia mpya ya malisho inaitwa JUNCAO, hii imeonesha mafanikio makubwa duniani. Ndugu zetu wa China tunaendelea nao na majadiliano.

Mheshimiwa Spika, hii itakwenda kujibu hata yale maeneo ya Longido, Monduli, Kiteto yenye kuonesha ile hali ya ukame na kwako Kongwa tunataka tufanye ni sehemu ya kwanza kabisa ya kwenda kupanda hii JUNCAO na hii JUNCAO itaenda kuondoa ile Kongwa wheats inayoonekana pale kama maua meupe hivi, lakini kumbe ni mtihani ule. (Makofi)

Nataka nikuhakikishie ng’ombe akiiona JUNCAO anaikimbilia yeye mwenyewe, tumejipanga kuhakikisha tunashirikiana na wenzetu watafiti na wengineo ili kuleta teknolojia hii itakayokwenda kujibu kilio cha malisho cha wafugaji wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho, nakushukuru sana, waarabu wanapenda sana wale mbuzi wadogo wadogo wa Masai breed, nawaombeni sana Waheshimiwa Wabunge tunaleta kopa ng’ombe, lipa ng’ombe, kopa mbuzi, lipa mbuzi, nendeni mkahamasishe tuhakikishe kwamba wanataka wale mbuzi wa kilo saba mpaka kilo nane, hawataki mambuzi yaliyokomaa sana. Tafadhalini sana hii ni fursa tunataka tuwatoe Watanzania katika umaskini na tuweze kupandisha pato la Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri Abdallah Ulega, tunakushukuru sana kwa ufafanuzi ambao umeutoa na kwa matumaini ambayo tumetupatia Watanzania, umesema neno moja kunenepesha kaa. Kaa ananenepeshwa?

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana tena kwa fursa hii, biashara ya kaa fattening inaitwa kaa, sorry crab fattening kwa maana ya kwamba yule kaa tunachukua wakiwa wadogo wadogo kutoka kule baharini, kwa sisi watu wa kule Ukanda wa Pwani tunafahamu jambo hili. Kwa hiyo, wale wanaokotwa, tena unaokota, kwa muda mrefu sasa sisi watu watu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi tumekuwa tukikimbizana na Watanzania wanaotumia fursa ya kuwauzia Wachina wanahitaji sana tena wanahitaji sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa sisi tumeona kwa nini tukimbizane nao, tuwatengenezee utaratibu uliokuwa mzuri, watu wafundishwe, waokote wale kaa wakiwa wadogo wadogo, watengeneze majaruba kule pwani, wakishatengeneza yale majaruba, wanakula, tena wale ulaji wao huwawekei chakula chochote ni yale yale maji, law types na high types maji yakiingia na kukupwa tayari wewe unakuwa umenenepesha na unauza unapata pesa nyingi sana. (Makofi)