Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026

Hon. Dr. Paulina Daniel Nahato

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026

MHE. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi nami pia nichangie juu ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo. Nami nitajikita katika masuala ya afya. Awali ya yote napenda sana kuishukuru na kuipongeza Serikali katika ujenzi wa miundombinu ambayo imeifanya mpaka sasa katika masuala ya afya Na marekebisho mengi yaliyofanyika katika upatikanaji wa huduma ya afya, yaani huduma ya afya imekuwa bora zaidi.

Mheshimiwa Spika, napenda kuishauri Serikali kuwa, pamoja na kwamba tuna mambo mengi sana ambayo tunayaongelea, lakini suala la afya ni muhimu sana. Ninaomba kujikita katika sehemu ya kinga. Hili eneo la kinga au preventive au public health halijaangaliwa sana, yaani halijapewa kipaumbele sana kama tiba. Mambo mengi sana yanayoongelewa ni kuhusu tiba na siyo suala la kinga.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba magonjwa mengi yanazuilika. Kama tutaweza kuzuia magonjwa mengi, tutaweza kukuza uchumi; Tutapata watu ambao watakuwa na afya na wataweza kujikita katika masuala ya uchumi hasa tutakapojikita katika masuala ya kinga. Magonjwa mengi yanatibika. Magonjwa ambayo tunaita communicable diseases na non-communicable diseases, magonjwa yote tuseme.

Mheshimiwa Spika, hivyo basi, ili kuweza kufanikiwa katika eneo hili, kuna mambo matatu, kwa kifupi sana naomba kuishauri Serikali. Angalau kuwe na mipango ya aina tatu; mipango ya muda mfupi, mipango ya muda wa kati na mipango ya muda mrefu. Ninapoongelea mpango wa muda mfupi ni kwamba sasa ni kweli wananchi wengi vijijini elimu haiwafikii kuhusu visababishi vya magonjwa mengi. Matokeo yake, kunakuwa na mlundikano wa wagonjwa katika hospitali zetu, ambapo kama hao wananchi wetu watafikiwa na kujua vyanzo vya magonjwa mengi ni nini, wangeweza kujizuia, na hivyo, tuta-save fedha nyingi sana na tutafanya mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa sasa hivi ni kweli elimu inatolewa, lakini inatolewa kwenye televisheni na redio ambapo vijijini watu hawana hivyo vitu. Tufanye nini? Tufanye kila njia kuhakikisha kwamba wananchi wote hasa wa vijijini wanafikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ushauri wangu ni kwamba Wahudumu wa Afya wale walioko kule vijijini kule, Primary Health Care watumike kusambaza elimu ya kinga kwa wananchi wao. Watasambazaje? Ziko mbinu nyingi za kusambaza. Wale Wahudumu wanaweza wakaongea na wagonjwa asubuhi kabisa pale wanapofika kabla ya kupata huduma wakawaeleza, wale watu wakajua na hivyo wanaweza wakajikinga. Kwa mfano, magonjwa yanayotokana na maji machafu na minyoo na vitu kama hivyo, watu wanaweza wakajizuia tu. Kama ambavyo sasa hivi tumesambaza habari kuhusu Corona na watu wanajizuia.

Mheshimiwa Spika, katika Mpango wa muda wa Kati sasa, labda kuweza kuwajengea hawa Wahudumu uwezo wa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi mfupi (short trainings) ili hata wao wenyewe wajue namna ya kuongea na wananchi kuanzia chini mpaka kwenda juu. Faida yake ni kwamba, magonjwa yatapungua. Magonjwa yakipungua hata matumizi ya dawa yatapungua.

Mheshimiwa Spika, pia katika Mpango huo huo wa muda wa kati kuna suala la kuongeza watumishi na kuongeza utafiti. Tafiti zinafanyika, wanafunzi wanakwenda field, lakini hizi tafiti zinaishia kwenye Ofisi za Kata. Maana utafiti ukifanyika, ukimaliza kufanyika, report ndogo inatolewa inafikishwa Ofisi ya Kata au ya Kijiji, lakini zile tafiti zinawekwa tu kwenye madroo. Watafiti wakirudi mara ya pili, wananchi wanasema sisi tulikuwa hatujui, hawakupewa matokeo ya zile tafiti.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali iangalie kuhakikisha kwamba haya matokeo ya tafiti wananchi wanayapata. Kwa hiyo, msisitizo uwe kwenye Serikali za Mitaa kuhakikisha kwamba tafiti zinazofanywa na watafiti zinawafikia wananchi wote hasa wale wa chini. Basiā€¦

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)