Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, kwanza nachukua fursa hii kwa kukushukuru wewe kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia katika hotuba ya Wizara hii. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuitayarisha na kuiwakilisha hotuba hii katika Bunge lako kwa ufasaha mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Elimu na Mafunzo ya Uvuvi; nachukua nafasi hii kuipongeza Wizara kwa kuweka mpango huu mzuri katika nchi yetu ambao una manufaa kwa wavuvi wetu. Katika Hotuba ya Waziri, Ukurasa wa 89 – 90 imeeleza namna ya FETA kwa kushirikiana na NORGEES VEL ya Norway iliyofadhili kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya pamoja na mambo mengine lakini zaidi kufundisha stadi za ufugaji na biashara katika maeneo kadhaa ya nchi yetu. Hili ni jambo zuri ambalo linapaswa kushukuriwa na kupongezwa. Ushauri wangu katika jambo hili ni kwamba, Wizara ipanue wigo wa kueneza jambo hili katika maeneo mengi zaidi, hasa yale ya vijijini ambako kuna wavuvi ambao uwezo wao ni mdogo sana.

Mheshimiwa Spika, Migogoro Kati ya Wafugaji na Wakulima; tatizo la migogoro ya ardhi kati ya makundi haya makubwa katika nchi yetu bado ni kubwa. Ni vyema Wizara ikalichukulia jambo hili kwa uzito unaostahili ili kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.