Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Yosepher Ferdinand Komba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Spika, napenda nianze kuzungumzia barabara ya Amani – Muheza, zaidi ya kilometa 20 ambayo Serikali iliahidi kuiweka lami kwani Tarafa ya Amani yenye kata sita inategemea barabara hiyo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, kilimo, utalii na kadhalika, je, ni lini barabara ya Amani – Muheza itajengwa kwa kiwango cha lami?

Mheshimiwa Spika, barabara ya Muheza kwenda Magoroto inahitaji kuwekwa lami kwani ni barabara inayoenda kwenye mashamba ya michikichi ambayo ni maeneo yanayozalisha lakini pia Magoroto kiutalii (Magoroto Camp) ambayo inaingiza pato la halmashauri na nchi kwa ujumla. Je, ni lini barabara hii itajengwa kwa lami ikizingatiwa ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, Bandari Kavu Pangani na Kigombe. Kumekuwa na kuzuka kwa bandari kavu (bandari bubu), naomba kufahamu Wizara ina utaratibu gani wa kurasimisha bandari hizi ili ziweze kuwa chachu ya maendeleo kwa Wilaya za Muheza na Pangani.

Mheshimiwa Spika, minara ya simu; kuna tatizo kubwa la mawasiliano ya simu Tarafa ya Amani, Kata za Zirai, Misalai na Bwiti.