Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. WILLIAM T. OLENASHA: Mheshimiwa Spika, napenda kwanza kuwapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri na watendaji wa Wizara kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, napenda kuishukuru Wizara ya Ujenzi na Serikali ya Awamu ya Tano kwa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara katika jimbo la Ngorongoro, hususani barabara ya Loliondo - Mto wa Mbu inayojengwa kwa kiwago cha lami.

Mheshimiwa Spika baada ya pongezi hizo, naomba nieleze changamoto zilizopo katika Jimbo la Ngorongoro. Kwanza, ni kusimama kwa ujenzi wa barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu. Ujenzi wa barabara hii unasuasua kutokana na ukosefu wa fedha na uchelewashaji wa malipo kwa mkandarasi. Kwa sasa mkandarasi anadai zaidi ya shilingi bilioni 13. Kwa sababu cashflow isiyo nzuri, mkandarasi amelazimika kusimamisha ujenzi kwa kiasi kikubwa kuanzia tarehe 19/4/2019. Mkandarasi amelazimika pia kupunguza wafanyakazi 300 kwa sababu ya kukosa fedha za kuendelea na ujenzi. Ucheleweshaji huu wa malipo utaendelea kufanya mradi kuchelewa kukamilika. Tunaomba Wizara ifanye malipo mapema ili ujenzi uweze kuendelea.

Mheshimiwa Spika, pili, kukwama kwa miradi ya mawasiliano ya simu za mkononi, Tarafa ya Ngorongoro. Tunashukuru sana Wizara kupitia Mpango wa Mawasiliano kwa Wote kwa kutuletea miradi ya mawasiliano katika Wilaya ya Ngorongoro ikiwemo ile inayotekelezwa ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, eneo la matumizi mseto ya ardhi lenye vijiji 25 na wakaazi wapatao 95,000.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kupatikana msaada huu wa Serikali, ujenzi wa minara umekwama kwa muda mrefu kutokana na vikwazo vya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ikiwepo taratibu za Tahmini ya Mazingira (EIA) inayochukua muda mrefu kukamilika. Baadhi ya miradi ambayo imeshindwa kuendelea kwa wakati ni pamoja na ile ya Embakaay (Naiyobi), Sendui (Alaililai) na Nainokaroka inayojengwa na kampuni ya Halotel.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara itupie jicho miradi ya mawasiliano ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwani wananchi wanakosa huduma muhimu inayotolewa na Serikali. Wizara iangalie usahihi wa miradi midogo kama miradi kufanyiwa tathmini kubwa ya mazingira (EIA) na katika njia inayochukua muda mrefu.

Mhe Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache, naomba kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.